MANDONGA KUMPA RAIS SAMIA MKANDA WA UBINGWA WA PST,AMSHUKURU KWA KUWAJALI MABONDIA NCHINI
Bondia wa ngumi za kulipwa nchini, Karim Mandonga ametoa shukrani kwa Rais wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuunga mkono jitihada za mabondia katika mchezo wa ngumi za kulipwa hapa nchini.
Mandonga ametoa shukrani hizo Jijini Dar Es Salaam wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa Habari katika Hoteli ya Makunduchi Villa iliyopo Kigamboni Jijini humo,siku chache mara baada ya kutwaa mkanda wa ubingwa wa Afrika Mashariki na kati PST.
Mandonga ambaye alifanikiwa kushinda mkanda wa Ubingwa wa PST kufuatia mkuchapa kwa pointi Kenneth Lukyamuzi kutoka Uganda Mwezi Novemba 2024 alisema Mkanda huo atauotoa kama Zawadi kwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kama sehemu ya shukrani zake.
Alisema kuwa aliupokea 'Mkono' wa Rais Dkt Samia alioutoa kwa Mabondia nchini katika siku ya pili ya sikukuu ya Krismasi (boxing day) kama Zawadi ya kufunga mwaka kwa Mabondia na wadau wa sekta ya mchezo wa ngumi ambapo na yeye (Mandonga) pia alipewa
"Kwa kuwa amekuwa ni Rais anayetambua umuhimu wa sekta ya michezo hasa mchezo wa ngumi hapa nchini Mimi nitatoa Mkanda huu nilioshinda kama sehemu ya kumshukuru kwani Sina Cha kumlipa kwa Makubwa aliyofanya kwetu kama mabondia hivyo pia Namuomba Mungu ampe nguvu mama na amuongezee siku za kuishi ili aendelee kutuunga Mkono na tunamuombea pia katika kipindi chake kingine tena kama Rais na Sasa ni muda wa kwenda na mama Samia"alisema.
Hata hivyo Mandonga amewashauri vijana nchini kuwa na nidhamu ambapo wanataka kuingia katika mchezo wowote ule kwani nidhamu humfilisha mtu mbali zaidi na kufikia malengo yake.
Naye Mkurugenzi wa Makunduchi Villa Hotel iliyopo Kigamboni, Mohammed Haji alisema wao kama hoteli wamekuwa wakifanya jitihada za kumsapoti bondia Karim Mandonga na hata alipokuja na jambo la Mama walifurahia kwani wao wanaamini utendaji wa Rais Dkt Samia
"Sisi tulianza kumsapoti Mandonga tangu alipoanza ngumi ya SGR kwa ajili ya kusapoti mradi wa reli ya kisasa ambapo alipigana katika hoteli yetu na kushinda na hata aliponipigia simu kuniambia kuwa ana jambo la mama nlimwambia akija Dar aje hapa hotelini kwa ajili ya kuzungumza jambo hilo na watanzania "
Alisema hoteli hiyo yenye mazingira ya kisasa pia itawapokea wageni ambao watapitia Dar Es Salaam kuelekea katika michuano ya Afcon itakayochezwa kule Jijini Arusha mwaka 2027 kwani hoteli hiyo ina mandhari ya kuwavutia wateja wake na iko katika eneo tulivu kwa Mapumziko huku akiwakaribisha wananchi wa Jiji la Dar Es Salaam na viunga vyake kuitembelea hoteli hiyo na kupata huduma zenye hadhi.
Comments