KORIE WAMPA SHAVU SHILOLE,ATANGAZWA KUWA BALOZI WA MAFUTA HAYO

KORIE WAMPA SHAVU SHILOLE,ATANGAZWA KUWA BALOZI WA MAFUTA HAYO.


Msanii na mfanyabiashara mashuhuri hapa nchini Tanzania, Zuwena Mohammed maarufu kama Shilole, ametangazwa rasmi kama balozi wa Mafuta ya Kupikia Korie, akiongeza mvuto wake mkubwa kwa chapa hiyo iliyoboreshwa kwa mwonekano mpya na vifungashio vipya.

Shilole aliongoza uzinduzi wa vifungashio vya nusu lita na robo lita vya mafuta ya Korie, hatua inayolenga kuwafanya Watanzania wengi zaidi kupata mafuta ya kupikia yenye ubora kwa urahisi.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo kubwa, Shilole alionyesha furaha yake na kusema:
"Korie Kipochi kimefika kwa mikono sahihi na kwa wakati sahihi! Hata unapomaliza mafuta ghafla, Korie Kipochi ni suluhisho la haraka—kamili kwa dharura za jikoni."

Vifungashio hivi vipya, vilivyotengenezwa kwa mifuko laini ya plastiki chini ya jina "Kipochi", vimebuniwa kwa bei nafuu ili kuwafikia walaji wa kipato cha chini" amesema Shilole

Lengo ni kusaidia familia kupunguza gharama za chakula bila kuathiri ubora wa bidhaa wanazotumia.

Kwa zaidi ya miaka 20, mafuta ya Korie yamekuwa sehemu ya familia nyingi nchini Tanzania, na hatua hii mpya inathibitisha dhamira yake ya kuwafikia watumiaji wote.

Meneja wa Mauzo wa Murzah Wilmar, watengenezaji wa mafuta ya Korie, Steven Ford, alisisitiza kuwa kampuni hiyo inajali afya za walaji wake:
"Lengo letu ni kuhakikisha Watanzania wote wanapata mafuta bora na salama kwa bei nafuu, hasa wale wanaohitaji chaguo rafiki kwa mfuko wao."

Aliongeza kuwa ni muhimu kwa walaji kununua bidhaa zilizoidhinishwa na TBS, akirejelea tukio lililotokea Yombo Dovya, ambapo mafuta yasiyo salama yalileta madhara makubwa kwa afya za watu.
"Kwa kutumia mafuta yaliyoidhinishwa, mnalinda afya zenu na kuepuka bidhaa bandia hatari," Ford alionya.

Ingawa masharti ya Mkataba wa  ushirikiano wa Shilole na Murzah Wilmar yamebaki kuwa siri, jambo moja liko wazi—ushawishi wake utaisaidia Korie Kipochi kufika katika kila nyumba Tanzania, kuhakikisha kila familia inapika kwa mafuta salama na yenye ubora wa hali ya juu.

Comments