NANI KUMRITHI KINANA CCM?NI JANUARI 18-19 MWAKA HUU,NI KATIKA MKUTANO MKUU WA CHAMA HICHO
NANI KUMRITHI KINANA CCM?NI JANUARI 18-19 MWAKA HUU,NI KATIKA MKUTANO MKUU WA CHAMA HICHO
Chama Cha Mapinduzi CCM kinatarajia kufanya Mkutano Mkuu ambao pamoja na mambo mengine umebeba ajenda tatu ikiwemo ya kujadili na kupampata mrithi wa Makamo Mwenyekiti Tanzania bara.
Mkutano huo unatarajiwa kufanyika Januari 18 hadi 19 mwaka huu jijini Dodoma kutokana na kujiuzulu kwa aliyekua makamo Mwenyekiti Bara ndugu Abdulrahman Kinana.
Akizungumza na waandishi wa habari Makao Makuu ya CCM katika ukumbi wa White House jijini Dodoma leo, Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, CPA Amos Makalla, amesema mkutano mkuu huo utakuwa na ajenda tatu.
Alizitaja ajenda hizo ni kujaza nafasi ya Makamu Mwenyekiti Tanzania Bara kufuatia kujiuzulu kwa aliyekuwa akishika nafasi hiyo Ndugu Abdulrahman Kinana,kupokea kazi za Chama kuanzia mwaka 2022 hadi 2025 pamoja na kupokea taarifa ya utekelezaji Ilani ya uchaguzi ya CCM.
Ameeleza kuwa taarifa hizo za utekelezaji ilani ni kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ)
Kuhusu mchakato wa kumrithi Kinana, amesema mrithi wa nafasi hiyo anatarajiwa kupatikana baada ya kamati kuu kuwasilisha mapendekezo ya jina kwa halmashauri kuu kisha halmashauri kuu kuwasilisha jina hilo kwa wajumbe wa mkutano mkuu kwa ajili ya kupigiwa kura.
Comments