NI MABATI ZONE TANZANIA TENA,YAGAWA VIFAA VYA MICHEZO BUGURUNI VETERANS FC

 


Mtendaji Mkuu wa Mabati Zone Tanzania Mikidadi Athumani (katikati) na wawakilishi wa Timu ya Buguruni Veterani wakionesha jezi watakazotumia kwenye Ligi ya Maveterani inayotarajia kuanza hivi karibuni


Mtendaji Mkuu wa Mabati Zone Tanzania Mikidadi Athumani akionyesha mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam bidhaa aina ya mabati ambayo kampuni hiyo imekuwa ikizalisha,kukuza na kusambaza kote nchini Wakati wa kuikabidhi vifaa vya michezo timu ya Buguruni Veterani.


Mtendaji Mkuu wa Mabati Zone Tanzania Mikidadi Athumani akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Wakati wa kuikabidhi vifaa vya michezo timu ya Buguruni Veterani.


NA MWANDISHI WETU

Kampuni ya Mabati Zone Tanzania imeikabidhi timu ya Buguruni Veterani vifaa vya michezo vyenye thamani ya shilingi milioni 3.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Januari 24, 2025, jijini Dar es Salaam katika hafla ya makabidhiano hayo, Mtendaji Mkuu wa Mabati Zone Tanzania, Mikidadi Athumani, alisema vifaa hivyo vitatumika na timu ya Buguruni Veterani kwenye Ligi ya Maveterani inayotarajiwa kuanza hivi karibuni.

Athumani alivitaja vifaa hivyo kuwa ni jezi za timu hiyo za nyumbani na ugenini, jezi za magolikipa na makocha, pamoja na mipira watakayotumia kwa maandalizi ya ligi hiyo, ambayo miongoni mwa timu zitakazoshiriki ni Maveterani wa Simba na Yanga.

"Lengo la kukabidhi vifaa hivi vya michezo kwa timu ya Buguruni Veterani ni kuwawezesha kushiriki kwenye Ligi ya Maveterani. Licha ya kuwa mimi ni CEO wa Mabati Zone Tanzania, pia ni mchezaji wa soka," alisema Athumani na kuongeza:

"Hivyo, tunataka vifaa hivi viwe chachu kwa timu yetu kufanya vizuri kwenye ligi hii. Nina imani watafanikiwa kwa kuwa wana wachezaji wenye vipaji na wanaendelea kujiandaa kwa bidii ili kuimarisha ushindani wao."

Aidha, Athumani alisema kuwa kupitia udhamini huo, kampuni ya Mabati Zone Tanzania itazidi kutambulika kwa Watanzania, huku wakiahidi kuendelea kusaidia wale wanaohitaji msaada wa aina hiyo.

Mtendaji huyo alitumia fursa hiyo kutoa wito kwa wanamichezo wengine kushiriki kikamilifu kwenye masuala ya michezo kama sehemu ya kuendeleza vipaji.

Katika hatua nyingine, akizungumzia bidhaa za mabati zinazotolewa na kampuni hiyo, Athumani aliwahimiza Watanzania kujenga kwa kutumia mabati bora kutoka Mabati Zone Tanzania, ambayo ni imara, bora, na yanayodumu kwa muda mrefu bila kupoteza ubora wake.

Alieleza kuwa wateja wa kampuni hiyo husafirishiwa mabati bure hadi majumbani mwao, hata kama wapo mikoani.

"Tuna mabati ya aina mbalimbali, yakiwemo ya migongo mipana. Kampuni yetu ni kubwa, na tunashauri wateja wetu kuezeka kwa mabati bora kutoka Mabati Zone Tanzania," aliongeza Athumani.

Alisema kuwa kampuni hiyo imekuwa ikitoa elimu kuhusu aina mbalimbali za mabati ili Watanzania waweze kuchagua mabati bora kwa ajili ya kuezeka.

Kwa upande wake, Kocha wa timu ya Buguruni Veterani, Omary Mbweze, aliishukuru Mabati Zone Tanzania kwa msaada huo wa vifaa vya michezo kwa ajili ya Ligi ya Maveterani.

Kocha huyo alitumia fursa hiyo kutoa wito kwa wadau wengine kujitokeza na kusaidia timu ya Buguruni Veterani.

Akizungumzia maandalizi ya ligi hiyo, Mbweze alisema ana matumaini makubwa kwamba timu yao itafanya vizuri kwa sababu wamefanya usajili wa wachezaji wenye vipaji. Pia aliwataka wakazi wa Buguruni kujitokeza kwa wingi kuishangilia timu yao wakati wa mechi.

Mawasiliano Mabati Zone Tanzania: 0766 616 676

Comments