POLISI YAMNASA HOUSE GIRL ALIYEIBA WATOTO WA BOSI WAKE DAR,YUMO MGANGA WA KIENYEJI.

POLISI YAMNASA HOUSE GIRL ALIYEIBA WATOTO WA BOSI WAKE DAR,YUMO MGANGA WA KIENYEJI.




NA MWANDISHI WETU 

Jeshi la polisi Kanda maalum ya Dar Es Salaam limemtia Mbaroni mfanyakazi wa ndani (house girl) kwa tuhuma za wizi wa watoto wawili.

Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es salaam Kamanda wa polisi wa Kanda hiyo SACP Jumanne Muliro amesema kukamatwa kwa mfanyakazi huyo wa ndani kumeenda sambamba pia na kukamatwa kwa mganga wa kienyeji ambaye akishirikiana na binti huyo.


Amesema mnamo January 12,2025 walipata taarifa za kuibwa kwa watoto wawili wadogo mvulana na msichana mmoja miaka mitano na mwingine minne na dada wa Kazi za ndani akishirikiana na mganga wa kienyeji ambapo watoto hao ni wa  familia ya Mohammed Kasim Mkazi wa Tandika,Temeke

"Baada ya kupata taarifa hizo poliisi ilifanya upelelezi na kufanikiwa kuwapata watoto wote wawili nyumbani kwa mganga wa kienyeji aliyefahamika kwa jina la AbdulKarim Sharif miaka 43, maneno ya Kimara Baruti,Ubungo"amesema SACP Muliro

Amesema Watoto hao walifanyiwa Vipimo vya afya na kubainika afya zao ziko salama na Kisha kukabidhiwa kwa wazazi wao huku watuhumiwa wakiendelea kuhojiwa juu ya dhamira iliyowapelekea kuwateka watoto hao ilikuwa ni ipi.

Aidha Jeshi hilo limetoa wito kwa wananchi kujua historia za wasaidizi wa ndani ambao huwaajiri kwa kuepuka tabia za kuchukua wasaidizi wa Kazi za nyumbani wasiojua historia na tabia zao,kwani kufanya hivyo ni hatari iliyojificha.

"Kuchukua msaidizi wa ndani bila kujua eneo alilotokea Wala historia yake ni sawa na kuweka bomu ndani"alisema.

Katika hatua nyingine Jeshi hilo limesema kuwa limepata taarifa ya picha mjongeo(video) ikionyesha askari wawili wa usalama barabari wakifanya matendo ambayo ni kinyume na Kazi ya polisi na askari hao tayari wamekamatwa na kuwekwa mahabusu kabla ya kuchukuliwa hatua za kinidhamu.

"Jeshi halitovumilia kitendo chochote Cha kulidhalilisha Jeshi au vilivyo kinyume na maadili ya Jeshi,hivyo Jeshi halitovumilia vitendo hivyo vinavyochafua taswira ya Jeshi"alisema 

Comments