ABOOD ALIPONGEZA JESHI LA POLISI MORO,URATIBU MAFUNZO YA UDEREVA
ABOOD ALIPONGEZA JESHI LA POLISI MORO,URATIBU MAFUNZO YA UDEREVA
MBUNGE wa Jimbo la Morogoro mjini, Abdul Azizi Abood amelipongeza Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro kitengo cha usalama barabarani kwa kuratibu mafunzo ya udereva wa pikipiki na bajaji kwa vijana wasio na leseni katika Manispaa hiyo
Abood ametoa pongezi hizo leo Februari 11, 2025 wakati wa zoezi la utoaji vyeti lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kikosi cha Usalama barabarani mara baada ya mafunzo hayo kukamilika.
Kwa upande wake Mkuu wa usalama barabarani Mkoa wa Morogoro SP Gabriel Chiguma amesema, lengo la kutoa mafunzo hayo ni kuwapa ujuzi wa kuendesha vyombo vya moto na kuwapa uelewa juu ya sheria, alama na michoro ya usalama barabarani.
Akida Jumbe, dereva wa bajaji Manispaa ya Morogoro amesema mafunzo hayo yatamfanya asiogope tena Polisi wa usalma barabarani kwani itakuwa chachu kwake kufuata sheria kwa sababu amezifahamu.
Comments