KIKAO CHA RCC CHAPITISHA BAJETI YA BILIONI 848.7 YAPITISHWA RC CHALAMILA ATOA NE

  KIKAO CHA RCC CHAPITISHA BAJETI  YA BILIONI 848.7 YAPITISHWA RC CHALAMILA ATOA NENO





Na PrayGod Thadei,

Dar es salaam.

Ili kuhakikisha Mkoa wa Dar Es Salaam unaendelea kuwa miongoni mwa Mikoa yenye maendeleo makubwa hapa nchini,Kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Dar es Salaam (RCC) kwa kushirikiana na Bodi ya Barabara ya Mkoa huo,kimepitisha rasimu ya bajeti ya mwaka wa fedha 2025/26 yenye jumla ya shilingi Tsh. 848,792,144,255. Bajeti hiyo inatarajiwa kuimarisha miundombinu na kuendesha shughuli mbalimbali za maendeleo ndani ya mkoa.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kikao hicho, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, alisema bajeti hiyo itakuwa chachu ya maendeleo katika mkoa, hasa kwenye miradi ya barabara, usafiri na huduma za kijamii.

"Bajeti hii inalenga kuboresha huduma muhimu kwa wananchi, kulipa mishahara, na kuhakikisha miradi ya miundombinu inatekelezwa kwa wakati. Tumeunda pia kamati maalum itakayofuatilia mwenendo wa mtandao wa barabara ili kuhakikisha changamoto zilizopo zinashughulikiwa kwa haraka," alisema Chalamila.

Katika kikao hicho, wajumbe walikubaliana kuanzisha Kamati ya Utendaji itakayohakikisha bajeti inatekelezwa kwa ufanisi, huku wakisisitiza umuhimu wa uwazi na uwajibikaji katika matumizi ya fedha za umma.

Bajeti hii inatajwa kuwa hatua muhimu kwa mkoa wa Dar es Salaam katika kuhakikisha maendeleo endelevu na kuboresha mazingira ya kibiashara, usafiri, na ustawi wa wananchi.


Comments