MAFIA BOXING YAMLETA ULINGONI MTOTO WA MATUMLA,YASEMA ITAENDELEA NA 'KNOCK OUT YA MAMA' MPAKA KUMALIZIKA KWA UCHAGUZI.

 MAFIA BOXING YAMLETA ULINGONI MTOTO WA MATUMLA,YASEMA ITAENDELEA NA  'KNOCK OUT YA MAMA' MPAKA KUMALIZIKA KWA UCHAGUZI.




 NA MWANDISHI WETU 

Kampuni ya Mafia boxing Promotion imesema kuwa itaendelea kuandaa mapambano ya mchezo wa ngumi za kulipwa hapa nchini maarufu kama 'Knok out ya mama' kama sehemu ya kurejesha shukrani kwa Serikali.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa kampuni hiyo Ally Zayumba alipokuwa akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar Es Salaam kuelekea pambano la Knock out ya Mama msimu wa 3 ambalo linatarajiwa kufanyika February 28 mwaka huu katika ukumbi wa Magomeni city center Jijini humo.


"Kutokana na Kazi ambazo Rais,Dkt Samia amekuwa akizifanya hasa kukuza michezo na kuliendesha vyema Taifa la Tanzania sisi kama watanzania tumaeamua kumlipa kwani hata ukiangalia makusanyo ya Kodi yameonezeka na miradi mingi inafanyika hivyo tukaamua kumlipa kwa kuja na kaulimbiu knock out ya mama ili kumuunga mkono"

Zayumba amesema kuwa mapambano ya  Knock out ya mama yatakwenda mpaka mwishoni mwa uchaguzi wa mwaka huu ambapo ni sehemu ya shukrani za kampuni ya Mafia boxing promotion kwa Rais Samia.

Amesema katika knock out ya mama msimu wa 3,kutakuwa na mapambano (bout) 13 ambapo Pambano kuu (main card) litakuwa ni la Ameir Rashid ambaye ni mtoto wa aliyekuwa bondia maarufu nchini Rashid Matumla Matumla ambaye atazichapa dhidi ya  bondia kutoka nchini Namibia,Paulo Amavila

Aidha amewataka watanzania kujitokeza kwa wingi katika kushuhudia Pambano hilo la kukata na shoka ambalo pia litatanguliwa na mapambano mengine kadha wa kadha.

Naye mdau wa mchezo huo ambaye pia ni msanii wa bongo fleva,Shetta amepongeza jitihada za kampuni ya Mafia boxing Promotion katika kuandaa mapambano ya mchezo wa ngumi za kulipwa kwani yamerejesha Imani kwa wananchi juu ya mchezo huo na Kuona kuwa ni mchezo kama michezo mwingine na ni ajira kwa vijana.

Nao baadhi ya mabondia akiwemo bondia Ameir Rashid Matumla amesema kuwa ataendeleza kile ambacho alikuwa akikifanya kwa ukubwa zaidi kwani anafanya Kazi katika mazingira mazuri kupitia Mafia boxing hivyo kuwataka watanzania kujitokeza kwa wingi February 28 kushuhudia Pambano lake ambalo litakuwa na raundi 8.

Comments