SERIKALI IMEONDOA CHANGAMOTO WALIZOKUTANA NAZO WANAWAKE KATIKA UONGOZI – BI. BAHATI MTONO.

 SERIKALI IMEONDOA CHANGAMOTO WALIZOKUTANA NAZO WANAWAKE KATIKA UONGOZI – BI. BAHATI MTONO.


📌 Asema Siku ya Wanawake Duniani ilianzishwa mwaka 1975 na Umoja wa Mataifa

📌 Asema nishati safi ya kupikia inachagiza ukombozi wa kiuchumi kwa wanawake


Mkurugenzi Msaidizi wa Sehemu ya Usimamizi wa Rasilimali Watu katika Wizara ya Nishati, Bi. Bahati Mtono, amesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeondoa changamoto walizokutana nazo wanawake katika umiliki wa ardhi na masuala ya uongozi.


Akizungumzia historia ya harakati za wanawake kuelekea maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, Bi. Mtono alisema:


"Historia inaonesha kuwa tangu miaka ya 1910, kulikuwepo na harakati mbalimbali za wanawake kupigania haki zao. Mwaka 1975, Umoja wa Mataifa ulianzisha rasmi Siku ya Wanawake Duniani kwa lengo la kupigania haki za wanawake na kuhakikisha usawa wa kijinsia."


Ameeleza kuwa lengo la kuanzishwa kwa siku hiyo ni kuhamasisha dunia kutambua haki za wanawake na kuhakikisha wanashiriki kikamilifu katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi.


Kuhusu nafasi ya Wizara ya Nishati katika kusaidia wanawake, Bi. Mtono amesema taasisi zilizo chini ya wizara hiyo, kama Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), zinajitahidi kuongeza idadi ya wanawake wahandisi kupitia miradi mbalimbali, ikiwemo mradi wa TAZA.


Ameipongeza Serikali kwa juhudi zake za kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia, akisema kuwa mpango huo una lengo la kuhakikisha asilimia 80 ya Watanzania wanatumia nishati safi ifikapo mwaka 2034.


"Kupitia programu hii, mwanamke anakwenda kukombolewa kiuchumi kwa kuokoa muda wa kutafuta nishati mbadala na hivyo kushiriki kikamilifu katika shughuli za kijamii na kiuchumi," amesema Bi. Mtono.


#nishatisafi #sikuyaan

awake #usawa #maendeleo

Comments