UPENDO WA RAIS SAMIA,AMWACHIA MWANAFUNZI KUKALIA KITI CHAKE MKUTANONI TANGA.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Magila ya Muheza Ester George Barua ambaye alimruhusu akalie kiti chake cha Rais kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa CCM Jitegemee Wilayani Muheza Mkoani Tanga tarehe 27 Februari, 2025. Rais Dkt. Samia alifurahishwa na Mwanafunzi huyo wa Shule ya Sekondari ya Serikali ya Kata (Magila Sekondari) wakati akielezea mafaniko ya Serikali ya Awamu ya Sita kwa Lugha ya Kingereza.
KUHUSU UZINDUZI WA USAMBAZAJI WA NISHATI SAFI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizindua usambazaji wa Nishati safi ya kupikia kwa Mkoa wa Tanga katika viwanja vya CCM Jitegemee kabla ya kuwahutubia wananchi wa Muheza mkoani humo tarehe 27 Februari, 2025.
Comments