WANAFUNZI WA KIKE SOMENI MASOMO YA SAYANSI ILI MUWE WAHANDISI: ENG UPENDO HAULE
WANAFUNZI WA KIKE SOMENI MASOMO YA SAYANSI ILI MUWE WAHANDISI: ENG UPENDO HAULE
Na Mwandishi wetu.
Mwenyekiti Mstaafu wa Taasisi ya Wahandisi Tanzania, Mhandisi Upendo Haule ametoa wito kwa Wanafunzi wa kike ngazi ya Msingi na Vyuo Vikuu kupenda kusoma masomo ya Sayansi ili waweze kuwa Wahandisi.
Mhandisi Upendo ametoa rai hiyo leo Februari 28,2025 jijini Dar es salaam wakati akizungumza na Waandishi wa habari kuelekea maadhimisho ya siku ya Wahandisi na Uhandisi Duniani yatakayo fanyika Machi 4,2025 ambapo Kitaifa yatafanyika Mkoani Arusha.
"Kitaifa kutakua na Mkutano Mkuu ambao utafanyika Mkoani Arusha ambapo umeandaliwa chini ya Wizara mama,Wizara ya Ujenzi"amesema
Nakuongeza kuwa "Lakini sambamba na hilo upande wa Taasisi ya Wahandisi,tutakua na Kongamano ambalo tutalifanya hapa Dar es salaam katika chuo cha Teknolojia Dar es salaam (DIT) likihusisha vyuo mbalimbali na Wahandisi wanaoweza kushiriki.
Aidha Mhandisi Upendo ambaye pia ni Mhandisi mbobezi wa mradi wa Mkongo wa Taifa kutoka Kampuni ya Mawasiliano Nchini Tanzania( TTCL) amesema kuwa lengo kubwa la kongamano hilo ni kuhabarisha umma pamoja na wanafunzi wa vyuo kuonesha umuhimu wa uhandisi na kusherehekea sherehe ya Wahandisi na uhandisi Duniani.
Amesema kuwa Kongamano hilo litakua na mawasilisho mbalimbali yatakayokua yanazungumzia Wahandisi na teknolojia mbalimbali zinazoendelea za uhandisi.
"Sambamba na hilo tutakua na maadhimisho mengine maeneo mbalimbali ambayo yataendana na kutembelea mashule(school Visit),kwa lengo la kuhamasisha wanafunzi wa uhandisi" amesema
Nakusisitiza kuwa "Tumeamua kufanya Kongamano hili pale DIT na sio sehemu nyingine kwa lengo la kuhamasha uhandisi na kuwaonesha sisi Wahandisi tuliyopo lakini pia kuwahamasisha Wahandisi waliopo vyuoni.
"Tumeamua kwenda kwenye vyuo ili wao watuoneshe wanafanya nini,na sisi pia tuwaoneshe tunafanya nin,lakini mwisho wa siku tuweze kuhakikisha tuna ongeza wahandisi."
Ameaema kwamba katika maadhimisho hayo ya siku ya Wahandisi na uhandisi Duniani watatembelea shule za Msingi na Sekondari ili kuweza kuwaibua nakuwafanya wakae sawa kupata uelewa mzuri ili wasiache uhandisi.
"Kauli mbiu ya Mwaka huu kwa mujibu wa kimataifa ambayo ipo chini ya UNESCO, "shaping our future through engineering"maana yake nikuhakikisha kwamba tunakua na dunia endelevu yenye kustahimimili kupitia uhandisi" amesema
Nakuongeza kuwa "yaani Dunia yetu ya Sasa itakuaje hapo baadae kupitia uhandisi?..,Je uhandisi tunaoufanya ni stahimilivu?..,Je upande wa Mazingira ususani uhandisi tunaoufanya unalinda Mazingira?..,Mitambo tunayoizalisha inalinda Mazingira?..maana yake ni kwamba huu uhandisi wetu usiharibu Mazingira".
Comments