BANDARI KAVU YA KWALA MKOANI PWANI IMEPUNGUZA MSONGAMANO WA MALORI GERSON MSIGWA
BANDARI KAVU YA KWALA MKOANI PWANI IMEPUNGUZA MSONGAMANO WA MALORI GERSON MSIGWA.
Na Mwandishi wetu.
Pwani.
Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa amesema kuwa kwa sasa uzalishaji wa kiwanda cha SinoTan Park kilichopo kibaha mkoani pwani kinaendelea kuzalisha bidhaa mbalimbali Nchini huku. kimeweza kuajiri vijana zaidi ya 1000 huku serikali ikiwa imetenga baadhi ya maeneo katika kuzalisha kongani za viwanda Nchini.
Akizungumza na Waandishi wa habari Kwenye bandari ya Kwala mkoani pwani msemaji Mkuu wa serikali Gerson Msigwa amesema kuwa kiwanda cha SinoTan kilichopo kibaha mkoani pwani kinaendelea kuzalisha bidhaa mbalimbali zikiwemo majokofu, Nguo, na vifaa huku serikali kupitia wizara ya uchukuzi na mamlaka ya bandari Tanzania inaendelea kukuza miradi mingine ikiwemo bandari na viwanda huku makontena Zaidi ya 700 yamepokelewa kutoka kwenye bandari hiyo kavu iliyopo kwala mkoani pwani.
"Uwekezaji katika sekta ya viwanda ni sehemu muhimu iliyoleta matokeo chanya katika mapinduzi ya uchumi Nchini huku mapato kutoka viwanda ikiwa kiasi cha shilingi Tirioni mbili katika miaka minne ya Rais DKt Samia huku ajira laki 5 zikiwa zimeongezeka na miradi mbalimbali zaidi ya 1982.
Aidha mapato tunayopata tunaenda kuzalisha bidhaa Nchini huku tukipunguza idadi ya kununua kutoka nje ya nchi hivyo takwimu kwa sasa inaonesha kuwa kutoka January 2025 hadi February tumeweza kuzalisha miradi mingi Nchini."Amesema Msemaji Msigwa"
Mkoa wa pwani umeweza kupokea miradi mbalimbali ikiwemo viwanda vya chakula, matunda na nguo hivyo vijana kutoka Nchini Tanzania wataweza kupata ajira na kuweza kuzalisha zaidi ya Trioni moja.
Serikali Tumeweza kujenga bandari hii kutokana na kupunguza msongamano wa makontena kwenye bandari nyingine ikiwemo bandari ya Dar es salaam lengo likiwa ni kuweza kuhudumia wafanyabiashara huku bandari hiyo ikiwa na uwezo wa kuzalisha Makontena zaidi ya 30,0000 huku serikali ikiendelea na upanuzi wa bandari hiyo ambayo inaenda kupokea zaidi ya makontena 30.0000
Comments