BANDARI YA KWALA NI MKOMBOZI SEKTA YA USAFIRISHAJI KWA TAIFA: MSIGWA
BANDARI YA KWALA NI MKOMBOZI SEKTA YA USAFIRISHAJI KWA TAIFA: MSIGWA
Msigwa ameyasema hayo Leo March 16,2025 wakati akizungumza na waandishi wa Habari waliofanya ziara katika bandari hiyo sambamba na kutembelea eneo maalum la viwanda (kongani ya Viwanda) katika eneo la uwekezaji wa Viwanda la Sino Tan.
Amesema kuwa bandari hiyo ambayo ipo umbali wa takribani kikomita 90 kutoka Bandari ya Dar Es Salaam itasaidia wawekezaji mbalimbali kuhifadhi mizigo yao ambapo Kwa mwaka ina uwezo wa huhudumia Hadi makontena laki 3 Kwa mwaka.
"ndugu waandishi wa Habari eneo hili la bandari hii kavu ya Kwala lipo Karibu kabisa na Reli ya kisasa ya SGR na Ile ya MGR na itahudumia takribani makontena 823 kwa siku ambapo pia ina uwezo wa kuhifadhi asilimia 30 ya mizigo yote inayoshuka katika Bandari ya Dar Es Salaam" amesema.
Aidha amesema kuwa Serikali imewekeza kiasi Cha Shilingi bilioni 83 Hadi kufanikisha kukamilika kwa mradi huo ambapo maeneo yote yanayoingia na kutoka katika bandari hiyo yamejengewa miundombinu rafiki ikiwemo upatikanaji wa barabara yenye kiwango Cha zege,umeme,maji na pia kuwepo kwa Reli ambayo inaisafirisha makontena hayo kutoka bandarini.
- Get link
- X
- Other Apps
Comments