CUF YAUKATAA MUUNGANO NA CHADEMA,YAANDAA ILANI KWA KUTIMIA AKILI MNEMBA (AI)


 

Chama cha wananchi-CUF kimesema kuwa uchaguzi mkuu wa mwaka huu,ufanyike baada ya kufanyika kwa marekebisho ya sheria ya tume huru ya Taifa ya Uchaguzi,INEC


Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar Es Salaam Leo jumapili March 2,2025 Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho,Prof Ibrahim Lipumba amesema kuwa Kutokana na hali iliyoonekana kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa,kutoridhisha hivyo uchaguzi wa Rais,wabunge na madiwani unapaswa kufanyika tu mara baada ya marekebisho yanayoitambua tume huru ya Taifa ya Uchaguzi.

Aidha Prof Lipumba amesema kuwa pia Serikali inabidi kuwa na sera Bora katika nyanja mbalimbali ikiwemo katika sekta ya afya kwa kutoa huduma Bora za afya kwa watanzania wa viapato vyote,pamoja na kuondoa utaratibu wa kuzuia miili ya wanaofariki wakiwa wanaendelea na matibabu baada ya ndugu zao kushindwa kulipa fedha wanazodaiwa.

"Serikali ikiwekeza vizuri kwenye sekta ya afya itatatua changamoto mbalimbali kwa wananchi ikiwemo upatikanaji wa huduma za afya kiurahisi"amesema Lipumba.

Amesema kuwa chama hicho kitaendelea na sera yake ya haki sawa na furaha kwa wote mpaka ambayo ina dhamira kuu ya kujenga uchumi shirikishi,kuongeza ajira,huduma Bora za matibabu na elimu,na kuongeza tija itakayoleta Mapinduzi kwenye Kilimo pamoja na uongezaji wa thamani kwenye madini ili kuendelea kuwavutia wawekezaji hapa nchini.

Aidha amesema timu maalum ya chama hicho inaendelea kuandaa ilani ya chama hicho ambapo pia watatumia akili mnemba (AI)katika uandaaji wa ilani hiyo ya Uchaguzi ya Chama wananchi-CUF.


"timu inayondaa ilani ya Uchaguzi naipongeza sana kwa kuweza kutumia akili mnemba na nadhani itakuwa ni ilani Bora sana hivyo natoka wito kwa watu wote kuendeleza sera ya haki sawa na furaha kwa wote na watanzania pia waendelee kutambua kuwa uchaguzi una gharama zake,hivyo watuunge mkono kwenye azma yetu ya kuleta mabadiliko"amesema Pro Lipumba.

Kuhusu mashirikiano Prof Lipumba amesema kuwa wao kama chama wanapenda muungano lakini wana tahadhari kubwa kwani hata walipoungana katika chaguzi zilizopita waligeukwa na wenzao.

"Kuna vyama vinakuja kutaka mshirikiane Kimkakati,siyo kwamba wanataka mshirikiane kweli bali wanataka mshirikiane ili wakumalize wewe"amesema.

Ameongeza kuwa ushirikiano inabidi utoe faida kwa vyama vyote na si kwa chama kimoja pekee kwenye muungano huo.

Comments