DOYO KUANZA HARAKATI ZA KUWANIA URAIS KESHO DAR,KUCHUKUA FOMU
DOYO KUANZA HARAKATI ZA KUWANIA URAIS KESHO DAR,KUCHUKUA FOMU
Katibu Mkuu wa Chama cha National League for Democracy (NLD), Mhe. Doyo Hassan Doyo, ambaye alitangaza rasmi nia ya kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mnamo Machi 14, 2025, mjini Morogoro, anatarajiwa kuchukua rasmi fomu ya kugombea nafasi hiyo tarehe 20 Machi 2025.
Kwa mujibu wa kanuni za NLD, sura ya pili inamtaka mtia nia kuchukua fomu ya kugombea ndani ya siku 14 kabla ya mkutano mkuu ili kukidhi matakwa ya kikanuni. Hatua hii ni muhimu katika safari ya Mhe. Doyo kuelekea kinyang’anyiro cha Urais kupitia tiketi ya chama hicho.
Shughuli ya uchukuaji fomu itafanyika katika ofisi za NLD zilizopo Tandika, Mtaa wa Lituhi, Jijini Dar es Salaam, mkabala na msikiti wa watoto yatima, kuanzia saa 4:00 asubuhi. Wanachama wa NLD na waandishi wa habari wanakaribishwa kushiriki katika tukio hili muhimu la kihistoria.
#DoyoKwaUrais #NLD #Uchaguzi2025 #Demokrasia #Tanzania
Comments