FEDHA ZA KUJENGA ARENA ZIMEPATIKANA:MSIGWA
Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa amesema Serikali tayari imeshapata fedha kwa ajili ya kuanza kwa ujenzi wa Arena ambao utaichukua shughuli za michezo,sanaa na burudani.
Msigwa ameyasema hayo katika mkutano wake na waandishi wa Habari uliofanyika Jijini Dar Es Salaam na kuongeza kuwa tayari eneo limeshapatika katika eneo la kawe na walikuwa katika mchakato wa kutafuta fedha.
Amesema kuwa fedha hizo ambazo ni za mkopo wa masharti nafuu zilipatikana baada ya ziara ya Rais Dkt Samia nchini Korea.
"Baada ya ziara ya Korea Rais Dkt Samia alipata mkopo nafuu wa takribani dola milioni mbili na baadaye akatoa bilioni 400 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa Arena hiyo ili wasanii waanze kufanya Kazi zao za kiburudani"amesema
Aidha ameongeza kuwa Arena hiyo inatarajiwa kuingiza zaidi ya watu elfu kumi na nne kwa wakati mmoja.
Hata hivyo Msigwa ameongeza kuwa pia wameshapata eneo kujenga Kijiji Cha sanaa,ambacho kitajengwa katika eneo la Kwala lilopo Mkoani Pwani.
Hilo limejiri Kufuatia wasanii wa sanaa za maonyesho na muziki nchini kupaza sauti kuhusu suala la kupata uwanja maalum (Arena) wenye viwango vya kimataifa ambao utatumika kuonyeshea kazi zao na hata kuandaa shughuli mbalimbali kama vile event za wasanii wa kimataifa, tuzo na matamasha mengine ya burudani, vilio vimefika mahali pake.
Kwenye Mkutano na Waandishi wa Habari ambao umefanyika mchana huu wa leo, Msemaji Mkuu wa Serikali @gersonmsigwa amesema "Arena inakuja, Wasanii mumshukuru sana Rais, @samia_suluhu_hassan tumekuwa na mipango ya muda mrefu kuhusu mradi huu lakini hatimaye Mhe Rais amepata fedha, tumepata Mkopo wa masharti nafuu na zimetengwa pesa kwaajili ya ujenzi wa Arena na Kijiji cha Filamu! Fedha zikija tutaanza ujenzi wa Arena mara moja."
"Tuna ugomvi mkubwa na CAF, hawapendi kuona tunautumia Uwanja wa Benjamin Mkapa kwa matukio ya nje ya michezo, lakini ukweli ni kwamba hatuna pa kuyapeleka, Mipango yetu ni kujenga Arena yenye uwezo wa kuingiza watu Elfu 15, kama tutapanga kuongeza ama kupunguza tutajua hapo mbele lakini mipango yetu ni hiyo!"



Comments