MIAKA MINNE YA RAIS DKT SAMIA INA MAFANIKIO LUKUKI:ALLY HAPI

 



Katika Kongamano la kumpongeza Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutimiza miaka 4 ya uongozi wake madarakani, Mhe Ally Hapi ambaye ni Katibu Mkuu Jumuiya ya Wazazi CCM amesema Dkt Samia anastahili pongezi kwa kupambana na adui maradhi.


"Baba wa Taifa aliwahi kusema kwamba tunao maadui wakubwa watatu, ujinga, umasikini na maradhi, inawezekana tuna maadui wengi lakini hao ni wakubwa watatu. Mhe Rais Dkt Samia amefanya kazi kubwa sana katika kupambana na adui maradhi, katika kipindi chake cha miaka 4 moja ya ajenda ambazo zimemsukuma sana ni kuhakikisha Watanzania walioko mijini na vijijini kwanza wanapata huduma za afya karibu na maeneo wanayoishi, pili kuhakikisha kwamba vituo vya afya viwe vizurna vyakutoa huduma za kisassa"


"Katika miaka 4 Dkt Samia amejenga Hosputali za Wilaya 129, Vituo vya afya 485 katika kata, katika kipindi chake kila Halmashauri imepata magari mapya ya kisasa mawili! Wenzetu majirani Wakenya walikuja kujifunza namna ambavyo Dkt Samia ame-transform sekta ya afya." -Ally Hapi


Comments