Mtemvu wa Kibamba Ajitokeza Kujiandikisha, Kuboresha Taarifa Zake Daftari La Kudumu La Mpiga Kura
Mtemvu wa Kibamba Ajitokeza Kujiandikisha, Kuboresha Taarifa Zake Daftari La Kudumu La Mpiga Kura
Na Mwandishi Wetu
DAR ES SALAAM: MBUNGE wa Jimbo la Kibamba, Wilayani Ubungo, Dar es Salaam, Issa Jumanne Mtemvu amejitokeza Katika Kituo cha Kibwegere Shule, Mtaa wa Kibwegere Kata ya Kibamba mkoani Dar es Salaam kŵa ajili ya kujiandikisha na kuboresha taarifa zake katika Daftari la kudumu la Mpiga kura ili aweze kupata fursa ya kuchagua viongozi kwenye uchaguzi
Hili linakwenda aambamba na kuandikisha wapigakura wapya lakini linalenga kuboresha pia taarifa za wapiga kura wa zamani wakiwemo wale waliopoteza kadi zao .
Kwa mujibu wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amesema uandikishwaji huo utafanyika kwa siku saba umeanza jana Machi 17 na utakamilika Machi 23, 2025.
Amesema uandikishwaji huo unawahusu waliotimiza miaka 18, pia wale waliopoteza kadi zao ama kuharibika watapatiwa nyingine.
Comments