ZIARA YA RAIS SAMIA ARUSHA YALIPA,MSIGWA ASEMA WANANCHI WA MIKOA YA KASKAZI KUNUFAIKA NA HUDUMA YA MAJI SAFI.

 ZIARA YA RAIS SAMIA ARUSHA YALIPA,MSIGWA ASEMA WANANCHI WA MIKOA YA KASKAZI KUNUFAIKA NA HUDUMA YA MAJI SAFI.






NA MWANDISHI WETU.
Serikali imesema kuwa ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mkoani Arusha imekuwa na manufaa makubwa kwani miradi mbalimbali ya maendeleo ilizinduliwa katika Mkoa huo na Mkoa Jirani wa Kilimanjaro.

Akizungumza na waandishi wa Habari Mkoani Pwani, Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa amesema kufuatia ziara hiyo ambayo Rais Dkt Samia aliifanya kuanzia March 9 mwaka huu ni dhahiri kwamba Sasa watanzania wana Imani kubwa na Dkt Samia.

Amesema Kupitia ziara hiyo Rais Samia alizindua mradi wa maji wa Same-Mwanga-Korogwe ambao utakuwa Mkombozi kwa wananchi wa maeneo hayo kwa kuwapatia maji safi na salama na utazalisha Lita za ujazo takribani milioni 103.

Aidha amesema kuwa kwenye mradi huo wa maji kiasi Cha Shilingi bilioni 406 zimetumika kwa kulipa wakandarasi ambapo tayari katika maeneo ya Wilaya za Same na Mwanga wananchi wameanza kupata huduma za maji safi na salama.

Hata hivyo Msigwa ameongeza kuwa ili kuhakikisha Mikoa ya Morogoro,Pwani na Dar Es Salaam inaendelea kupata maji ya uhakika,Serikali inaendelea na ujenzi wa bwawa la Kidunda lililopo Mkoani Morogoro ili kuhakikisha kunakuwa na upatikanaji wa maji muda wote ambapo bilioni 335 zitatumika na tayari mradi umefikia asilimia 28.

''kwwnye mradi huu wa bwawa la Kidunda pia mbali na wananchi kupata maji tunategemea kuzalisha umeme megawat 20 na baadaye utaunganishwa kwenye gridi ya Taifa na mradi huu unajumuisha utengenezaji wa tuta,njia ya kutokea maji na mtambo wa kufua umeme na kuusafirisha'' amesema Msigwa.

Comments