BOSS KWEZI AWATAKA WATANZANIA KUCHANGAMKIA FURSA ZA VIWANJA





Ardhi ni rasilimali muhimu sana kwa jamii,rasilimali hii inaweza kuwa urithi pekee usoyohamishika ulimwenguni.

Kwa kutambua hilo Vijana na watanzania kwa ujumla wametakiwa kujikita zaidi katika uwekezaji hususani wa ardhi kwani hupanda thamani kila siku ukilinganisha na vitu vingine.


 Wito huo umetolewa na Mkurugenzi mtendaji wa Boss Kwezi George Kwezi alipokuwa akizungumza na waandishi wa mtandao huu, ambapo amesema ardhi kila siku hupanda thamani tofauti na vitu vingine kama magari, ambavyo hushuka thamani baada tu ya kununua hivyo amesisitiza jamii kuona umuhimu wa kumiliki ardhi kwa wingi.


Boss Kwezi pia amesema kwa mtu anayetaka kununua kiwanja ama eneo ni lazima ajihakikishie kuwa muuzaji ni halali na si tapeli ili kuepusha migogoro inayoweza kujitokeza baadae.


"Kwa anaetaka kunua kiwanja nawashauri kunua kwa boss kwezi kwani ni mtu anayeaminika na mwenye gharama nafuu zaidi ya uuzaji wa viwanja hapa Tanzania".


"Viwanja vya boss kwezi hakuna mvamizi anayeweza kuvamia, kwanza hata matapeli wanaogopa kuvamia kwa boss kwezi kwani hata katika maeneo anayouza watu wanamfahamu".


"Mimi niliona watu wanatapeliwa sana kwenye ununuzi wa viwanja nikaona hiyo ni fursa ya kuja na kampuni ya uhakika ya uuzaji wa viwanja vya uhakika na vya gharama nafuu. 


Nimekuja kama suluhisho la matatizo ya watu kwani watu walikuwa wanatapeliwa wanauziwa mara mbili, wanakesi mahakamani wanapoteza muda na fedha zao, viwanja vya boss kwezi ni vya uhakika,vimepimwa na tunatoa hati ya umiliki na ndio maana hata kauli mbiu yetu ni viwanja vya uhakika".

Aidha amesema boss kwezi wana viwanja katika maeneo mbalimbali ndani ya jiji la Dar es salaam na Pwani na bei yake inaanzia Tsh laki nane mpaka milioni 3 unapata kiwanja,pia unaweza kulipa nusu ya bei na nyingine unamalizia kidogo kidogo.

Pia amewatoa hofu wale wanaoona maeneo kama Bagamoyo,Kibaha na Vikindu ni mbali na kusema kuwa maeneo hayo si mbali kwani miji inakuwa na kutanuka kila siku akitolea mfano maeneo kama Magomeni,Kariakoo,Kimara,Mbezi luis na Tegeta kote kulikuwa porini ila sasa ni mjini.

"Leo mkisema kibaha ni mbali kesho mtakuja kujilaumu kwa sababu hata Magomeni zamani ilikuwa porini hata Kimara ilikuwa ni porini, hata Mbezi napo palikuwa ni porini tu,iwapo msipoichangamkia hii fursa ipo siku mtakuja kumkumbuka boss kwezi".amesema

Comments