BOSS KWEZI MDHAMINI TAMASHA LA FILAMU ZA KISWAHILI LA KIMATAIFA

BOSS KWEZI MDHAMINI TAMASHA LA FILAMU ZA KISWAHILI LA KIMATAIFA




Ili kuhakikisha lugha ya kiswahili kupitia filamu inafika zaidi kimataifa,mfanyabiashara Boss kwezi adhamini tamasha la kiswahili  International swahili filmz festival tamasha ambalo limeandaliwa na wasanii wa maigizo ya Mzani wa mapenzi na Kombolela kwa lengo la kukuza lugha hiyo.

Akizungumza kuhusu udhamini wa tamasha hilo,Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya uuzaji viwanja na mashamha George Kwezi maarufu kama Boss Kwezi amesema kwa muda mrefu amekuwa akitamani kuona kiswahili kinakuwa kwani ndiyo lugha inayotambulika zaidi barani Afrika.

"Kwanza kabisa mimi ni Mtanzania mimi ni mwafrika na nimekuwa na chachu ya kupenda kiswahili kikue,kwani ndiyo lugha ambayo tunajidai,tunatamba nayo afrika kwahiyo ni livyosikia kuna watu wameamua kukuza ili kiende mbele zaidi nilivutiwa nikaona na mimi niweke mkono wangu katika kuhakikisha lugha yetu inakuzwa na kufika mbali zaidi".amesema

Comments