Mabati Zone Yasifu Mapinduzi ya Kibiashara ya Rais Samia – Yajipanga Kuinua Uchumi kwa Ushirikiano wa Kitanzania

 Mabati Zone Yasifu Mapinduzi ya Kibiashara ya Rais Samia – Yajipanga Kuinua Uchumi kwa Ushirikiano wa Kitanzania



NA MWANDISHI WETU 

Sekta ya ujenzi nchini Tanzania inaendelea kushamiri kwa kasi kubwa, huku wauzaji wa vifaa vya ujenzi wakizidi kuonyesha imani kwa serikali ya awamu ya sita.

 Mojawapo ya wadau wakubwa katika sekta hiyo ni kampuni ya Mabati Zone, inayojihusisha na uuzaji wa mabati ya viwango vya juu kwa bei rafiki kwa Watanzania.

Mikidadi Hassan Athumani, Mkurugenzi na kampuni hiyo na msambazaji wa mabati kupitia Mabati Zone na mfanyakazi wa kampuni ya Wachina ya Polaris, amesema serikali ya Rais Samia imefungua milango ya fursa kwa wafanyabiashara na wawekezaji kupitia maboresho ya sera za kodi na urahisishaji wa shughuli bandarini.

Mikidadi aliyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa Habari juu masuala mbalimbali ambayo kampuni hiyo imekuwa ikiyafanya 

“Kwa sasa mizigo inatoka kwa wakati bandarini, jambo ambalo linapunguza gharama na usumbufu kwa wafanyabiashara kama sisi. Mazingira ya biashara yameboreshwa, na hii imeongeza imani kwa wawekezaji,” alieleza Mikidadi.

Kampuni hiyo, licha ya kuwa huru bila kuhusishwa na kampuni yoyote ya uzalishaji, inawakaribisha wawekezaji watakaopenda kushirikiana nao katika kuzalisha mabati hapa nchini, hususani Watanzania. Lengo lao kuu ni kukuza uchumi wa nchi kwa kushirikiana na wadau wa ndani.


Kuhusu kampuni ya Mabati zone katika kukuza sekta ya michezo,Mikidadi alisema kuwa kampuni hiyo imekuwa ikiunga mkono jitihada za RAIS wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan katika sekta ya michezo kwa kuhakikisha inatoa msaada wa vifaa vya michezo kwa wanamichezo mbalimbali wa timu za mitaani.

Amesema kuwa wamekuwa kama moja ya wadhamini kwenye mashindano mbalimbali ya mpira wa miguu jijini Dar es salaam ikiwemo kudhamini na kuipatia vifaa vya michezo timu ya wachezaji wa zamani wa Klabu mbalimbali hapa nchini ya Buguruni Veterani.





Kwa upande wake, Meneja wa Mabati Zone, Bi. Jacquline Swai, amesisitiza kuwa kampuni hiyo inatoa mabati ya kila aina, yenye ubora wa kimataifa, na huduma rafiki kwa wateja wake. Amesema wateja wanaonunua kutoka kwao hupata ofa ya misumari bila malipo, usafirishaji wa bidhaa, pamoja na huduma ya kupata fundi wa kuezeka.

“Tunajali ubora wa bidhaa zetu na pia tunawajali wateja wetu. Hata zaidi, tunarudisha kwa jamii kwa njia ya misaada mbalimbali, kutembelea wagonjwa, yatima na wasiojiweza. Huu ndio moyo wa Mabati Zone,” alisema Jacquline.

Kwa mahitaji ya mabati, wateja wanaweza kuwasiliana kupitia:

0766 616 676
0665 508 173

Au kutembelea ofisi za Mabati Zone zilizopo Tabata Matumbi, Dar es Salaam.


#fursa
#mabatiyatanzania
#raisamiahassan
#hudumabora
#mabatzone
#uchumimbadala
#watanzaniawazalendo
#viwandavyaNdani
#tanzaniainajengwa

Comments