PROF.LIPUMBA ASHAURI SERIKALI KUFANYA UCHUNGUZI,KUPOTEA KWA WATU
PROF.LIPUMBA ASHAURI SERIKALI KUFANYA UCHUNGUZI,KUPOTEA KWA WATU
*Aiomba serikali kufanya uchunguzi na kutoa taarifa ili kuondoa malalamiko na kuleta matumaini ya amani kwa Wananchi.
*Amuomba Askofu Gwajima kupeleka orodha ya waliotekwa na vielelezo vyote ili uchunguzi ufanyike.
Na Mwandishi Wetu.
Chama Cha Wananchi (CUF) kimeiomba Serikali kulichukulia kwa umuhimu mkubwa suala la kutekwa,kupotea naku uawa kwa watu katika Mazingira ya kutatanisha.
Rai hiyo imetolewa leo Mei 29,2025 Jijini Dar es salaam na Mwenyekiti Taifa wa Chama hicho Profesa Ibrahim Lipumba wakati akifungua Mkutano wa siku mbili wa Baraza la Uongozi Taifa la Chama hicho.
"Tupo katika kikao hiki huku nchi yetu ipo katika majaribu makubwa,kuna malalamiko mengi ambayo yametokea kuhusiana na watu ambao inasemekana wametekwa,na hili suala limekua kadhia kubwa"amesema Prof Lipumba.
Nakuongeza kuwa "hivi karibuni Mchungaji Askofu Gwajima ameeleza kwamba yeye binafsi anaorodha ya watu 83 ambao wamepotea,wengine wamepoteza maisha,wengine hawajulikani walipo na hili ni kadhia kubwa kwa nchi yetu"
Aidha amesema ndani ya CUF suala la utekaji limekuwepo kwa muda,ambapo Mwaka 2017,diwani wa viti maalumu wa CUF aliyekua anaishi Maporoni Halmashauri ya Kibiti Bi.Ziada Salum Nongwa ambaye alikua mke wa diwani wa Maporoni Juma Ngachoka alikamatwa na watu ambao wali dhaniwa kuwa ni askari wa usiku na wakati huo akiwa na mtoto wa umri wa mwezi mmoja.
"Ziada alikamatwa akawekwa kwenye mtumbwi kwenye visiwa hivi vya kibiti mpaka leo hajaonekana,mme wake alitufahamisha na sisi tukaweza kuungana katika kuweza kuomba msaada wa kuweza kumtafuta na bwana Ngachoka aliandika barua hadi kwa Waziri Mkuu lakini mpaka leo Ziada hajapatikana na kuna wengine wengi kwamba walipotea katika kipindi hicho"amebainisha Profesa Lipumba
Aidha ameendelea kusema kuwa watu kama wanapotea,au wanachukuliwa bila taratibu kujulikana kitendo hicho moja kwa moja kinavunja ibara ya 8,14 na 15,ya katiba ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania ambayo inalinda ustawi na haki za kuishi za Mtanzania
Amesema kuwa kitokana na kuwepo kwa malalamiko hayo ni wajibu wa Serikali kutoa msimamo na kuyachunguza mambo hayo,huku akimuomba Mchungaji Gwajima apeleke orodha na taarifa zote alizonazo ili vyombo vya Dola viweze kuhakikisha vinafanya uchunguzi huru na kutoa taarifa.
Vilevile Prof.Lipumba amesema kwamba baada ya matukio ya watu waliofika kusikiliza kesi ya Mheshimiwa Tundu Lisu,kuna baadhi ya watu walikamatwa na pana shutuma kwamba wengine waliingizwa kwenye mambo ambayo hayastahiki.
"Mimi binafsi nimesononeka sana na kauli za mbunge wetu wa Pandani Bi. Mariam alizozitoa ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kana kwamba ana shabikia watu kuumizwa na kuteswa."amesema
Nakusisitiza" Tunapozungumzia haki sawa kwa wote,maana yake ni kwamba watu wasifanyiwe matendo mabaya,na yeye ni mbunge wa Pandani mwaka 2001 nadhani alikua mdogo sana lakini mambo mabaya yalitokea katika visiwa vya Pemba,
sisi kama wana CUF ni watu ambao tuna amini katika haki sawa kwa wananchi wote hatuwezi kushabikia watu kuteswa,kunyanyaswa,mbunge anasema "watu waende wakibebwa wakitumia mitungi ya gesi"hizo ni kauli ambazo kwakweli zimenisikitisha, zimenifadhaisha,kwakweli sio msimamo wala sio sera za Chama Cha CUF.
Amesema kwamba Sera za chama Cha CUF ni sera za kuheshimu haki za binadamu na umuhimu wa haki sawa kwa Wananchi wote.
Katika hatua nyingine Profesa Lipumba amesema kuwa vyama vya siasa vilitegemea uchaguzi Mkuu wa safari hii,baada ya mazungumzo waliyofanya ndani ya baraza la vyama vya siasa unaweza ukasimamiwa vizuri baada ya kuwa impatikana tume huru ya uchaguzi(INEC) ambayo inawatendaji wake,lakini matumaini hayo hawakuweza kuyapata.
"Pamoja na hayo kuna mambo ambayo yanaweza yakaboreshwa kuelekea kwenye uchaguzi mkuu,kwanza daftari la kudumu la wapiga kura linapokua limeandaliwa washiriki wote katika uchaguzi hususani vyama vya siasa viweze kupata nakala ya daftari la wapiga kura."amesema
Nakuongeza" Mwaka 2005 tulipata daftari la kudumu la wapiga kura,lakini mwaka 2020 hatukupata daftari hilo,pia kuna kasoro ambazo zinavunja hata Sheria za hivi sasa kwamba kunakuwa na kura feki wakati wa uchaguzi,hivyo hatuhitaji kuwepo kwa kura feki safari hii
Comments