TANESCO YAZINDUA KAMPENI YA UHAMASISHAJI ULIPAJI MADENI NA ULINZI WA MIUNDOMBINU YA UMEME

 TANESCO YAZINDUA KAMPENI YA UHAMASISHAJI ULIPAJI MADENI NA ULINZI WA MIUNDOMBINU YA UMEME





Dar es salaam, 19 Juni 2025 –

SHIRIKA la umeme Tanzania, (TANESCO) limetangaza rasmi uzinduzi wa kampeni ya kitaifa yenye lengo la kuhamasisha wateja kulipa madeni yao ya umeme kwa wakati pamoja na kulinda miundombinu ya umeme. 

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo leo June 19,2025 Kaimu Mkurugenzi wa mawasilano na huduma kwa wateja na wa shirika hilo Bi Irene Gowelle amesema Kampeni hiyo, yenye kaulimbiu isemayo “ lipa deni,linda miundombinu Tukuhudumie",inazingatia pia ukaguzi wa mita zote, ikiwemo LUKU na za malipo kabla, ili kuboresha ufanisi na kuimarisha huduma kwa wananchi.

Kampeni hii inalenga kuhamasisha wateja wa malipo ya baada kuhakikisha wanalipa madeni kabla ya hatua za kisheria kuchukuliwa na pia kutoa motisha kwa wateja wanaofuatilia matumizi yao na kulinda miundombinu yetu.”  amesema

Bi. Gowelle pia alisisitiza kuwa ukusanyaji wa madeni na ulinzi wa miundombinu ni jukumu la kila Mtanzania:

 “Tunatoa rai kwa wananchi kutoa taarifa kuhusu uhalifu wa wizi wa umeme au uharibifu wa miundombinu kwa kushirikiana na vyombo vya dola ili kupunguza athari za ukosefu wa huduma.”amesema.  

Aidha shirika hilo pia limetoa Rai kwa wateja wake kote nchini,ambao wanadaiwa kutoa ushirikiano kwa kulipa madeni yao kwa wakati na hivyo kutoathiri upatikanaji wa huduma ya umeme kwenye shughuli zao


Comments