HEMED NKUNYA AREJESHA FOMU KUOMBA RIDHAA KUWANIA UBUNGE JIMBO LA KAWE
HEMED NKUNYA AREJESHA FOMU KUOMBA RIDHAA KUWANIA UBUNGE JIMBO LA KAWE
NA MWANDISHI WETU
MJUMBE wa Kamati ya Uchumi na Fedha wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kata ya Mbweni Mpiji, Hemed Shabani Nkunya, amerejesha fomu ya kuomba ridhaa ya Chama kuwania ubunge Jimbo la Kawe wilayani Kinondoni, Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Juni 30, 2025 jijini Dar es Salaam baada ya kukabidhi fomu hiyo, Nkunya amesema ametimiza wajibu wake wa kidemokrasia na haki yake ya kikatiba kama raia mwenye wajibu wa kushiriki katika uongozi wa Taifa kwa kugombea nafasi ya uongozi.
Kwamba hadi sasa waliojitokeza kutia nia ya kugombea Ubunge katika Jimbo hilo ni wengi, na kwamba hata kama hatateuliwa na Chama yuko tayari kuunga mkono atakayeteuliwa.
Hata hivyo ameeleza kuwa baada ya kurejesha fomu hiyo kinachobaki ni kusubiri taratibu nyingine za Chama ili kuamua nani atakayepatiwa nafasi ya kuliwakilisha Jimbo la Kawe.
Nkunya, amekabidhi fomu hiyo kwa Katibu wa Jumuiya ya Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Amos Richard.
- Get link
- X
- Other Apps
Comments