IBRAHIM MHINA AJITOSA UBUNGE JIMBO LA KINONDONI, achukua fomu kuomba ridhaa ya chama.
NA MWANDISHI WETU
MBARAZA wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Kata ya Hananasifu Ibrahim Mhina amechukua Fomu ya kuomba ridhaa ya Chama chake kugombea Ubunge Jimbo la Kinondoni, Dar es Salaam
Akizungumza na waandishi wa habari leo Juni 30, 2025 mkoani Dar es Salaam baada ya kukabidhiwa fomu hiyo amesema amechukua fomu hiyo kutimiza wajibu wake wa kidemokrasia.
Mhina, amekabidhiwa fomu na Katibu wa Jumuiya ya Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Amos Richard.
Comments