Skip to main content

KASHASHA AREJESHA FOMU , UBUNGE JIMBO LA KAWE

 

KASHASHA AREJESHA FOMU, UBUNGE JIMBO LA KAWE


NA MWANDISHI WETU

WAKATI makada mbalimbali wakiendelea kuchukua na kurejesha fomu za kuomba kuwania nafasi mbalimbali za uongozi ikiwemo Ubunge na udiwani,Katibu wa Elimu, Malezi, Mazingira na Aya, Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kinondoni Mhandisi Jonson Kashasha  amerejesha fomu ya kuomba ridhaa ya Chama kuwania Ubunge Jimbo la Kawe wilayani Kinondoni, Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Juni 30, 2025 jijini Dar es Salaam baada ya kukabidhi fomu hiyo, Mhandisi Kashasha amesema ametimiza wajibu wake wa kidemokrasia na haki yake ya kikatiba kama raia mwenye wajibu wa kushiriki katika uongozi wa Taifa kwa kugombea nafasi ya uongozi.

Ameeleza kuwa baada ya kurejesha fomu hiyo kinachobaki ni kusubiri taratibu nyingine za Chama ili kuamua nani atakayepatiwa nafasi ya kuliwakilisha Jimbo la Kawe.

Kashasha, amekabidhi fomu hiyo kwa Katibu wa Jumuiya ya Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Amos Richard.

Comments