MBETO: KUWEPO KWA DEMOKRASIA KUMECHANGIA ONGEZEKO WANACHAMA KUJITOKEZA KUCHUKUA FOMU
MBETO: KUWEPO KWA DEMOKRASIA KUMECHANGIA ONGEZEKO WANACHAMA KUJITOKEZA KUCHUKUA FOMU
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
Kuwepo kwa demokrasia katika Chama cha Mapinduzi (CCM), kunatajwa kuchangia ongezeko la wanachama wanajitokeza kuchukua fomu kuomba ridhaa ya kukiwakilisha kwenye Ubunge, Udiwani na Wawakilishi katika Uchaguzi Mkuu ujao, Oktoba 2025.
Akizungumza na wanahabari, leo 30 Juni 2025, Katibu wa Kamati Maalum NEC Zanzibar, Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Khamis Mbeto Khamis alisema CCM ni chama kikubwa na kinaungwa mkono na makundi yote katika jamii.
Alisema pande zote za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, watu wa makundi yote wamejitokeza kuchukua fomu wakiwemo mamalishe, wasanii, boda boda na watu wengine hali inayoonyesha kuwa kinakubalika.
“Nawapongeza kwa mwitikio mkubwa kiasi hicho ingawa tulitarajia kutokana na kazi nzuri iliyofanywa na Mwenyekiti Dkt. Samia na Makamu wake, Dkt. Mwinyi inafanya wananchi waone CCM ni sehemu salama” alisema Mbeto.
Ametaka wanachama zaidi kujitokeza kuomba ridhaa ya chama kwani ndani ya CCM kuna fursa nyingi kuliko upinzani na hakuna mwenye hatimiliki ya uongozi, chama kinaangalia uwezo wa mtu bila kujali iwapo ni tajiri au maskini.
Pia amebainisha kuwa chama hicho kimeonyesha jinsi gani kinavyokubalika kwa vitendo kutokana na kutii maagizo ya chama ya kuwataka watia nia kwenda kwa utulivu kuchukua na kurudisha bila mbwembwe wala shamra shamra zozote.
- Get link
- X
- Other Apps
Comments