MUSLIM HASSANALI,AJITOSA UBUNGE JIMBO LA KINONDONI

 MUSLIM HASSANALI,AJITOSA UBUNGE JIMBO LA KINONDONI





NA MWANDISHI WETU.

Aliyewahi kuwa mgombea wa nafasi ya Ubunge Jimbo la Ilala mnamo mwaka 2015 kupitia Chadema,Muslim Hassanali na baadaye kujiunga na chama cha Mapinduzi CCM,leo amechukua fomu kuwania nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Kinondoni.

Hassanali amechukua fomu hiyo leo June 30,2025 katika ofisi za Wilaya  chama hicho zilizopo Kinondoni jijini Dar es salaam.

Akizungumza mara baada ya kuchukua fomu hiyo Hassanali amesema kuwa ana nia ya dhati ya kuomba ridhaa ili kuwania nafasi hiyo ya Ubunge huku akiamini kuwa chama chake kitampa fursa hiyo.


Hassanali anakuwa ni mmoja wa wanachama ambao tayari wametia nia na hatimaye kuchukua fomu ya kuomba ridhaa ya kuteuliwa kugombea nafasi ya Ubunge ndani ya chama hicho.

Zoezi la uchukuaji na urejeshaji wa fomu za kuomba ridhaa ya chama cha mapinduzi CCM lilianza June 28 na linatarajiwa kutamatika June 2,2025





Comments