Skip to main content

SALUM ISMAIL ATIA NIA KUGOMBEA JIMBO LA KAHAMA MJINI,AFUNGUKA MAZITO

 

SALUM ISMAIL ATIA NIA KUGOMBEA JIMBO LA KAHAMA MJINI,AFUNGUKA MAZITO


Mwenyekiti Mstaafu wa UVCCM Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa wa Dodoma Salum Ismaili Salum akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

NA MWANDISHI WETU

HUKU vuguvugu la kutaka nafasi za Ubunge na udiwani ndani ya chama Cha Mapinduzi likiendelea nchini  Mwenyekiti wa UVCCM Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa wa Dodoma Salum Ismaili Salum ametia nia kugombea Ubunge Jimbo la Kahama mjini mkoani Shinyanga.

Salum amebainisha hayo leo Juni 18, 2025  akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam ambapo amesema ametia nia kwa sababu Rais Samia ambeya ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ametoa fursa ya uongizi kwa vijana.

Amesema kuwa lengo la nia ya kugombea ni Kwa ajili ya kuwaketea maendeleo Wananchi wa Kibaha mjini kwani kupitia fursa nyingi zilizopo jimboni huko ikiwemo migodi ya Madini.

Hivyo amesema kuwa Juni 28 Mwaka huu atakuwa ni miongoni mwa wagombea watakao jitokeza kuchukua fomu.

Katika hatua nyingine Salum amekemea wanasiasa na wanaharakati wanaochochea uvunjifu wa Amani Nchini hivyo amesema kuwa watahakikisha wanapambana nao.

Aidha ametoa wito kwa Watanzania kumuunga mkono Rais Samia kutokana na mazuri aliyoyafanya.

Kwamba Wakati anapokea kijiti Cha uongozi baada ya kifo cha Rais Dkt. John Magufuli kulikuwa na miradi mingi ambayo ilikuwa ikiendelea.

Amesema kuwa kutokana na Mazingira hayo watu wengi walidhani Rais Samia asingeweza kuiendeleaa na kuikamilisha, hata hivyo ameitekeleza vizuri na kuikamilisha jambo ambalo linafanya Watanzania wamuunge mkono.

Amekemea watu wanaomkejeli na kumsema vibaya kwamba hawatawavumilia

Comments