SALVINA MSULA ACHUKUA FOMU KUOMBA RIDHAA YA CCM KUWANIA UDIWANI VITI MAALUMU KINONDONI

 SALVINA MSULA ACHUKUA FOMU KUOMBA RIDHAA YA CCM KUWANIA UDIWANI VITI MAALUMU KINONDONI



DAR ES SALAAM, JUNI 30,2025.

Mwenyekiti wa umoja wa wanawake Kata ya Mwananyamala, Salvina Msula maarufu kama Ligu, amechukua fomu ya kuomba ridhaa ili kugombea nafasi ya udiwani viti maalumu katika Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni.

Hata hivyo  Msula, ambaye amekuwa mstari wa mbele katika masuala ya uongozi wa mtaa na maendeleo ya jamii, ameonyesha nia ya kupanua wigo wa huduma kwa wananchi kupitia nafasi hiyo.

Hatua hiyo inaashiria nia yake ya kushiriki kikamilifu katika uongozi na kuwakilisha sauti za wanawake ndani ya baraza la madiwani la manispaa hiyo. 


Comments