CCM YALIPITISHA JINA LA MARIA SEBASTIAN KAMA MWANAMKE PEKEE,KINYANG'ANYIRO CHA UBUNGE KAWE,sasa kupigiwa kura za maoni

 



Mwenyekiti wa Uchumi, Uwezeshaji na Fedha UVCCM Taifa, Maria Alphonce Sebastian, Mwanamke Pekee Kupitishwa Kwenda hatua inayofuata ya  Kura za Maoni Kawe

Mwenyekiti wa Uchumi, Uwezeshaji na Fedha katika Kamati ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa, Bi Maria Alphonce Sebastian, amekuwa mwanamke pekee aliyepitishwa na kamati ya  Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuendelea na hatua ya kura za maoni katika Jimbo la Kawe, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa itikadi, uenezi na mafunzo wa chama hicho (CPA), Amos Makalla alipotangaza majina ya watia nia waliopitishwa kuelekea hatua inayofuata ya kura za maoni, alimtaja Bi Maria Sebastian kama mwanamke pekee ambaye ataendelea kuomba kura kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Jimbo la Kawe ili kuchaguliwa kama mgombea Ubunge wa jimbo hilo kupitia CCM kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, 2025.

Bi Maria Sebastian atapambana na wagombea wengine waliopitishwa na chama hicho, ambao ni pamoja na Ndugu Geofrey Anyonyesisye TIMOTH, Mwakilishi wa Sheria Adv. Leonard Tungaraza MANYAMA, Derek Kaitira MURUSURI, Elias John KOMBA, na Godwin John KAMALA.

Comments