JERUSA KITOTO,WENGINE SABA KUCHUANA KURA ZA MAONI JIMBO LA KINONDONI
Katibu wa itikadi,uenezi na mafunzo wa chama Cha mapinduzi (CCM),CPA Amos Makalla ametangaza majina ya walioteuliwa kwenda kura za maoni kupitia majimbo ya Mkoa wa Dar es salaam huku Mjumbe wa halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi CCM,tawi la Msisiri B lililopo Mwananyamala,Bi Jerusa Kitoto akiwa ni mmoja wa waliopendekezwa kuwania Jimbo la Kinondoni.
Kufuatia uteuzi huo Sasa Bi Jerusa KITOTO atachuana na wengine saba akiwemo Iddi Azan,Abas Tarimba Wilfred Elias NYAMWIJA
Michael Richard WAMBURA,Adv. Julieth Venant RUSHULI, Wangota Mussa SALUM na Zena Khalfani KIPUTIPUTI.
Bi Jerusa sasa ataingia katika mchakato wa kupita kwa wajumbe wa Jimbo hilo kijitambulisha na baadaye kushiriki katika mchakato wa kupigiwa kura na wajumbe hao ili kukiwakilisha chama hicho katika nafasi ya Ubunge wa Jimbo la kinondoni.
Comments