NKUNYA NDIYE MRITHI WA GWAJIMA?ATIA MGUU KAWE,ATEULIWA KUWANIA KURA ZA MAONI JIMBO LA KAWE


Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), CPA Amos Makalla ametangaza majina ya walioteuliwa kwenda kura za maoni kupitia majimbo ya Mkoa wa Dar es Salaam, huku Hemed Shabani NKUNYA, mfanyabiashara na mjumbe wa Kamati ya Uchumi na Fedha wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mbweni Mpiji mkoani Dar es Salaam, akiwa ni mmoja wa waliopendekezwa kuwania Jimbo la Kinondoni.

Kufuatia uteuzi huo, sasa Bw. Hemed NKUNYA atachuana na wengine saba akiwemo Geofrey Anyonyesisye TIMOTH, Adv. Leonard Tungaraza MANYAMA, Maria Alphonce SEBASTIAN, Derek Kaitira MURUSURI, Elias John KOMBA, Godwin John KAMALA na Philip Sospeter MATONDO.

NKUNYA sasa ataingia katika mchakato wa kupita kwa wajumbe wa jimbo hilo kujitambulisha, na baadaye kushiriki katika mchakato wa kupigiwa kura na wajumbe hao ili kukiwakilisha chama hicho katika nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Kawe.

Comments