CCM KUZINDUA KAMPENI ZAKE KESHO DAR,MAELFU KUKUTANA TANGANYIKA PACKERS
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinatarajia kuzindua rasmi kampeni zake kuelekea Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 29 mwaka huu, Agosti 28, 2025 katika Viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe, Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa chama hicho, Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni mgombea kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ataongoza ufunguzi huo akiambatana na mgombea mweza, Dkt. Emmanuel Nchimbi.
Uzinduzi huo utaashiria kuanza rasmi kwa kampeni za CCM, si katika kugombea kiti cha urais pekee, bali pia kinyang’anyiro cha kugombea ubunge na udiwani kwa walioomba nafasi hizo kupitia chama hicho tawala na kikongwe katika eneo hili la Afrika Mashariki.
Kwa ratiba hiyo, CCM kitakuwa chama cha kwanza kuzindua kampeni za kunadi sera zake kwa wananchi tangu Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) ilipotangaza tarehe ya kuanza kwa kampeni hizo.
Comments