MGOMBEA URAIS NA MGOMBEA MWENZA WAKE NLD KUPOKELEWA KWA KISHINDO ,DAR JUMAPILI

MGOMBEA URAIS NA MGOMBEA MWENZA WAKE NLD KUPOKELEWA DAR JUMAPILI



Baada ya kuteuliwa rasmi na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, mgombea wetu wa urais kupitia chama cha National League for Democracy (NLD), Mheshimiwa Doyo Hassan Doyo, akiambatana na mgombea mwenza wake Bi. Chausiku Khatibu Mohamed, watawasili jijini Dar es Salaam tarehe 31/08/2025.

Kupitia taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari  na  Mkurugenzi wa Habari na Mahusiano ya Umma, NLD    Pogora Ibrahim Pogora  Mapokezi rasmi yatafanyika katika Makao Makuu ya Chama, Tandika, Dar es Salaam, yakihudhuriwa na viongozi waandamizi wa chama, wanachama na wananchi mbalimbali.

Ambapo pia Viongozi wa wilaya zote za NLD kutoka mkoa wa Dar es Salaam,Wananchi kutoka mikoa ya Dar es Salaam na Pwani,pamoja na Waandishi wa habari na vyombo vyote vya habari, kuhudhuria kwa wingi katika mapokezi haya muhimu ya mgombea wetu na mgombea mwenza wake.




Comments