Skip to main content

MWENYEKITI INEC AKAGUA MAANDALIZI YA UCHAGUZI MKUU CHAMWINO NA MTERA

 

MWENYEKITI INEC AKAGUA MAANDALIZI YA UCHAGUZI MKUU CHAMWINO NA MTERA




Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Mheshimiwa Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele, leo Septemba 25, 2025, ametembelea Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino, mkoani Dodoma, katika majimbo ya Chamwino na Mtera, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kukagua maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.

Katika ziara hiyo, Jaji Mwambegele alipokea taarifa ya maandalizi ya uchaguzi kutoka kwa Msimamizi wa Uchaguzi wa Halmashauri hiyo, ikihusu uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani. Aidha, alikagua vifaa mbalimbali vya uchaguzi ambavyo tayari vimepokelewa na kuhifadhiwa kwa matumizi ya uchaguzi.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotangazwa na NEC, Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 unatarajiwa kufanyika Oktoba 29, mwaka huu.

Kaulimbiu ya Tume kwa uchaguzi huu ni: “Kura Yako, Haki Yako – Jitokeze Kupiga Kura.

Comments