BOLT YAADHIMISHA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA KWA KUTOA SAFARI ZA BURE KWA WATUMIAJI WAPYA
BOLT YAADHIMISHA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA KWA KUTOA SAFARI ZA BURE KWA WATUMIAJI WAPYA
Mageuzi ya usafiri wa mijini nchini Tanzania yanaendelea kuonesha jinsi teknolojia inavyorahisisha maisha ya kila siku na kupanua fursa za kiuchumi.
Katika maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja, kampuni ya Bolt imeangazia nguvu ya huduma za usafiri wa kidijitali kwa kutoa safari tatu za bure kwa watumiaji wapya — hatua inayolenga kufanya huduma salama na za kisasa kupitia programu kuwa rahisi kupatikana kwa Watanzania wengi zaidi na kuongeza imani kwa suluhisho za kidijitali.
Usafiri si suala la kuhama tu kutoka sehemu moja hadi nyingine, bali ni jambo la ujumuishi.
Huduma nafuu na bora za usafiri hutoa fursa ya kufikia elimu, huduma za afya na ajira — nguzo kuu za maendeleo ya kijamii. Kwa mujibu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), upatikanaji wa intaneti umefikia asilimia 72 kufikia Machi 2025, ukichochewa na ongezeko la umiliki wa simu janja na uelewa mpana wa matumizi ya teknolojia. Mabadiliko haya yamebadilisha namna wananchi wanavyopata huduma — kutoka sekta ya fedha hadi usafiri — na hivyo kuunda uchumi uliounganika zaidi.
“Kuenea kwa matumizi ya simu janja na intaneti kunamaanisha Watanzania wengi zaidi sasa wanaweza kutumia huduma za usafiri wa kidijitali ambazo ni salama, zinazofuatilika na zenye kuaminika zaidi kuliko njia zisizo rasmi,” alisema Dimmy
Kanyankole, Meneja Mkuu wa Bolt Tanzania na Kenya. “Kadri usafiri unavyokuwa wa kisasa zaidi, ndivyo watu wanavyopunguza muda wa kusafiri na kuongeza muda wa uzalishaji — jambo ambalo ni faida kwa uchumi.”
Hatua hii inaonesha jinsi majukwaa ya kidijitali yanavyounda mustakabali wa usafiri nchini Tanzania — mustakabali unaojikita katika usalama, upatikanaji, na ujumuishi kama nguzo kuu za miji inayosonga mbele.
MWISHO


.jpeg)
Comments