Skip to main content

HUDUMA ZA MOFAT KIASHIRIO CHA MATUMAINI MAPYA, SULUHU YA FOLENI DAR

 

HUDUMA ZA MOFAT KIASHIRIO CHA MATUMAINI MAPYA, SULUHU YA FOLENI DAR




Dar es Salaam
Mwenendo wa majaribio ya huduma za Mabasi yaendayo Haraka (BRT) katika njia ya Mbagala–Gerezani, unaoendeshwa na mwekezaji MOFAT Transport Company chini ya usimamizi wa DART, umeibua matumaini mapya ya kupunguza foleni jijini Dar es Salaam.
Katika ziara ya ukaguzi iliyofanywa na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini - LATRA, Oktoba 18, 2025 imebainika kuwa zaidi ya mabasi 200 yamewasili tayari, huku 37 yakiendelea na majaribio. Mabasi hayo yanatumia gesi asilia (CNG) na mifumo yake imekamilika katika karakana za Mbagala, hatua inayolenga kuboresha huduma na kupunguza uchafuzi wa mazingira.
LATRA imesema nauli ya majaribio itaendelea kuwa shilingi 750 hadi pale changamoto zote zitakaposhughulikiwa na huduma kuanza rasmi, ambapo nauli itapanda hadi shilingi 1,000.
Wakazi wa Mbagala wameeleza kuridhishwa na huduma hiyo, wakisema imepunguza muda wa safari na kuongeza tija katika shughuli zao za kila siku.
Mkurugenzi wa MOFAT, Abdulrahman Abdallah Kassim, ametoa wito kwa wananchi kulinda miundombinu ya mradi huo, akisisitiza kuwa ni uwekezaji wa vizazi vya sasa na vijavyo.

Comments