Mbeto amtaja Rais Dk Samia kiongozi shupavu Afrika Mashariki

 Mbeto amtaja Rais Dk Samia  kiongozi shupavu Afrika Mashariki 




Mwandishi  Wetu, Zanzibar 


Chama Cha Mapinduzi kimesema watu wanaojaribu kulifuja jina na uongozi wa Rais Dk Samia Suluhu  Hassan  hawatafikia malengo hayo kwasababu chini ya uongozi wake yapo  mengi mazuri ya kutajika yamefanyika kwa maslahi  ya Taifa. 


Pia  CCM kimeutaka upinzani kuushukuru utawala wa Awamu ya Sita kutokana na juhudi za  kufanikisha kupata  maridhiano na kufungua ukurasa mpya .



Mbeto Khamis  Mbeto , Katibu wa Kamati Maalum  ya NEC  Zanzibar ,  Idara ya Itikadi  ,Uenezi na Mafunzo ,ameeleza hayo ,huku akiutaka upinzani kuacha Siasa za ushabiki , chuki na jazba.


Mbeto  alisema wakati  Rais Dk Samia akiingia madarakani,aliikuta nchi  ikiwa katika mkwamo wa demokrasia,kudorora kwa biashara ,kutoaminiana na  kupwaya kwa mahusiano mema  na baadhi ya  nchi jirani.


Si hivyo  tu, alisema kulikuwa na malakamiko mengu toka  kwa Wafanyabiashara  wakubwa, Wa kati na Wadogo pia  Akiba za watu kupekuliwa kwenye Mabenki pamoja na baadhi  ya Wnasiasa wa Chadema  kukimbia nchi .


"Rais Dk Samia jina lake halitachafuliwa kwa hadithi za kutunga kwenye mitandao   ya kijamii. Ni kiongozi shupavu,muungwana anayependa maridhiano. Ni  kati ya viongozi  wachache  Afrika  wenye utashi na uthubutu alionao  "Alisema Mbeto


Aidha  ,Katibu  huyo Mwenezi  alisema mara baada ya kuapa na kuwa Rais, Dk Samia alihakikisha anashughulikia kadhia zote zilizotishia mpasuko na  mmomonyoko wa Umoja  wa Kitaifa .


'Leo kuna badhi ya  Wanasiasa  wasio na  kumbukumbu  wameshasahau  yaliowasibu akawafariji .  Serikali yake imekamilisha Miradi mikubwa ya  kimkakati na kuanzisha mengine pia imekamilika " Alieleza


Hata hivyo Mbeto alisema kutokana na juhudi za Serikali  yake na  hatua kubwa zilizofikiwa kimaendeleo , wapo waliodhani asingeifikisha nchi katika kilele cha maendeleo yaliopo.


"Kwa uungwana na kujali  utu ameanzisha  kanuni ya Nne  ilioleta mapatano ya kijamii na  kisiasa.Utawala wake umeruhusu mikutano  ya hadhara  .Dk Samia  ni mpenda haki na Mwanademokrasia jasiri "Alifafanua Mbeto

Comments