Watu wanne wakamatwa kwa kuendesha Televisheni Mtandaoni bila leseni.
Watu wanne wakamatwa kwa kuendesha Televisheni Mtandaoni bila leseni.


Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, kwa kushirikiana na mamlaka nyingine za kisheria, limefanikiwa kuwakamata watu wanne kwa tuhuma za kuendesha televisheni mtandaoni bila kuwa na leseni.
Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Kanda Maalum ya Polisi Dar es Salaam SACP Muliro Jumanne Muliro alisema kuwa operesheni hiyo ilifanyika kati ya Oktoba 3 hadi 10, 2025, na kufanikisha kukamatwa kwa watuhumiwa hao wanne.
Alisema waliokamatwa ni Japhet Alex Thobias na Joseph Augustino Mabwe, wakazi wa Sabasaba Ukonga, wanaodaiwa kumiliki kituo cha WISPOTI TV; Tegemeo Zacharia Mwenegoha, mkazi wa Tabata Ilala, mmiliki wa T.MEDIA TWO; na Elia Costantino Pius, mkazi wa Mbezi Juu Kinondoni, mmiliki wa COSTA TV.
Kamanda huyo alibainisha kuwa uchunguzi wa awali umekamilika na hatua za kisheria zinaendelea ili watuhumiwa hao wafikishwe mahakamani haraka iwezekanavyo.
Aidha, Jeshi la Polisi limewataka wananchi kuendelea kufanya shughuli zao kwa kuzingatia sheria, na limesisitiza kuwa halitasita kuwachukulia hatua wale wote watakaobainika kukiuka taratibu za kisheria.

.jpeg)
Comments