DAR CITY YAANDIKA HISTORIA – BAL 2026 KWA MARA YA KWANZA TANZANIA,YAREJEA NCHINI KIBABE

 

DAR CITY YAANDIKA HISTORIA –  BAL 2026 KWA MARA YA KWANZA TANZANIA,YAREJEA NCHINI KIBABE


Timu ya mpira wa kikapu ya Dar City Basketball imeweka historia kubwa baada ya kuwa timu ya kwanza kutoka Tanzania kufuzu kucheza fainali za BAL 2026 (Basketball Africa League).

Wachezaji pamoja na viongozi wa timu hiyo walisema hayo leo jijini Dar es Salaam mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (Terminal 3), ambapo waliwasisitiza kuwa licha ya kupoteza kwa pointi chache dhidi ya wapinzani wao, wamehitimisha hatua ya Elite 16 katika nafasi ya tatu—nafasi iliyowapa tiketi ya moja kwa moja kwenda fainali.

Aidha akizungumza kwa niaba ya wachezaji kapteni wa timu hiyo Hasheem Thabit,ameeleza kuwa kuwa mafanikio hayo yametokana na maandalizi madhubuti, umoja ndani ya timu, nidhamu, pamoja na mshikamano wa mashabiki. Wameahidi kuendelea kupambana katika hatua ya fainali huku wakilenga kuandika ukurasa mwingine wa kihistoria na kuinua zaidi mchezo wa kikapu nchini.

Hatua hii inaonesha wazi kuwa timu za Tanzania zina uwezo wa kushindana na timu bora barani Afrika, na inatarajiwa kuongeza hamasa mpya miongoni mwa vijana wengi wanaoingia kwenye mchezo wa kikapu

Comments