MWAKA 2026 NI MWAKA WA KUTANGAZA AMANI YA TAIFA :NABII EDMOUND MYSTIC
MWAKA 2026 NI MWAKA WA KUTANGAZA AMANI YA TAIFA :NABII EDMOUND MYSTIC
Na Mwandishi Wetu
MTUMISHI wa Mungu, Nabii Edmound Mystic wa Kanisa la Heavenly Image Manifest (HIM Church), ametoa wito kwa vijana wote nchini kusimama kama wasanii na Watanzania kwa ujumla katika kutangaza amani na haki kwa manufaa ya Taifa la Tanzania.
Nabii Mystic ametoa hiyo jijini Dar es Salaam mapema leo Desemba 31, 2025 masaa machache kabla ya kuelekea mkesha wa kuvuka 2025, MGEUKO unaofanyika katika viwanja vya Kenton, Sinza Africasana.
Amesema mkesha huo umeandaliwa kwa lengo la kuwakutanisha watu mbalimbali ili kuvuka mwaka mpya pamoja, huku akisisitiza umuhimu wa umoja, maridhiano na kumtazama Mungu kama msingi wa mabadiliko ya kweli katika maisha ya mtu binafsi na jamii kwa ujumla.
Akizungumza kuhusu mkesha huo, Nabii Mystic amesema kuwa mkesha huo ni “Usiku wa Kuwa Alama ya Mgeuko,” siku inayomweka mtu katika mtazamo mpya wa maisha.
Amesema katika maisha, mtu hawezi kuwa na tija katika jamii inayomzunguka au katika mwili wa Kristo endapo hajapitia siku ya mgeuko, ambayo huleta mabadiliko ya ndani yanayoakisi matendo na mwenendo mpya.
“Tumeandaa mkesha huu kwa sababu mtu akija kama alivyo, hatoki kama alivyokuja,” amesema
Aidha, Nabii Mystic amesema kuwa maisha yana majira mbalimbali, na kila majira mapya hubeba aina fulani ya mambo mapya, hivyo aliwaomba watu kutokubali kuishi katika majira yaliyopita.
Ameongeza kuwa si kweli kwamba mwaka mpya huwa mpya kwa kila mtu, bali mwaka huwa mpya pale mtu anaposhuhudia mabadiliko mapya yanayoingia katika maisha yake.
“Ili mwaka mpya uwe mpya katika maisha yako, ni lazima kutokee badiliko fulani katika maisha,” amesema.
Aidha ametoa wito kwa Watanzania kwenda na kujitokeza kwa kushiriki mkesha huo pamoja na kuwapeleka watu wenye changamoto na shida mbalimbali katika viwanja hivyo.



Comments