DUNIA,MEMBE NA WENGINE WANNE WAHUKUMIWA VIFUNGO HIVI KWA MAKOSA YA UBAKAJI NA ULAWITI DAR
DUNIA,MEMBE NA WENGINE WANNE WAHUKUMIWA VIFUNGO HIVI KWA MAKOSA YA UBAKAJI NA ULAWITI DAR
Dar es salaam
Peter Julius mkazi wa Mbezi Mwisho, Dunia Sadick maarufu kama Dunia mkazi wa Chanika, Rajab Rashid Goma mkazi wa Mwanagati, John Jacob Nyamahemba mkazi wa Mbagala, Abdallah Faustin mkazi wa Kibada pamoja na Abubakar Jumanne Membe maarufu kama Abuu mkazi wa Mbagala ni miongoni mwa watuhumiwa waliopatikana na hatia na kuhukumiwa vifungo vikali jela kwa makosa ya kubaka na kulawiti katika Mahakama mbalimbali za Dar es Salaam.
Kamanda wa jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam SACP Jumanne Muliro ametoa takwimu hizo wakati akizungumza na waandishi wa Habari bapo amesema hukumu hizo zimetolewa kati ya Desemba 2025 na Januari 2026 baada ya mahakama kuthibitisha ushahidi dhidi ya watuhumiwa hao katika kesi za makosa dhidi ya binadamu yanayochukiza jamii.
Kwa mujibu wa Polisi, Peter Julius amehukumiwa kifungo cha maisha jela na Mahakama ya Wilaya ya Ubungo kwa kosa la kulawiti, Dunia Sadick amehukumiwa miaka 30 jela na Mahakama ya Wilaya ya Ilala kwa kosa la kubaka, huku Rajab Rashid Goma akihukumiwa kifungo cha maisha jela na Mahakama ya Wilaya ya Ilala kwa kosa la kulawiti.
Pia John Jacob Nyamahemba amehukumiwa kifungo cha maisha jela na Mahakama ya Wilaya ya Temeke kwa kosa la kubaka, Abdallah Faustin amehukumiwa miaka 30 jela na Mahakama ya Wilaya ya Kigamboni kwa kosa la kubaka, wakati Abubakar Jumanne Membe akihukumiwa kifungo cha maisha jela na Mahakama ya Wilaya ya Temeke kwa kosa la kulawiti.
Ameongeza kuwa Polisi pia wameendelea kutoa elimu kuhusu usalama barabarani na sasa wanawaonya madereva wote wanaokiuka sheria, hususan wanaopita kwenye njia za mabasi ya mwendokasi, kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
Sambamba na hilo, Jeshi la Polisi limetambua kuwepo kwa mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika utakaochezwa Februari 1, 2026 katika Uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es Salaam kati ya Simba SC ya Tanzania na Esperance de Tunis ya Tunisia.
Jeshi la Polisi limewahakikishia mashabiki na wapenzi wa soka kuwa ulinzi na usalama utaimarishwa ndani na nje ya uwanja huo, huku likiwatakia mafanikio mema wawakilishi wa Tanzania, Simba SC.



Comments