MSIMU WA 2 WA GUARDIAN OF THE PEAK KUCHOCHEA UHIFADHI MLIMA KILIMANJARO

 MSIMU WA 2 WA GUARDIAN OF THE PEAK KUCHOCHEA UHIFADHI MLIMA KILIMANJARO





Na Mwandishi wetu,Dar es salaam

Kuelekea uzinduzi wa utayarishaji wa makala ya Guardians of The Peak Msimu wa Pili, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Filamu, Ndg. Emmanuel Ndumukwa  amesema Serikali itaendelea kuthamini mchango wa wadau wanaotangaza utalii hapa nchini.

Ameyasema hayo kwa niaba ya   Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania, Dkt. Gervas Kasiga katika Mkutano wa Waandishi wa Habari uliofanyika leo tarehe 14 Januari, 2025 katika ukumbi wa hotel ya King Jada, Kinondoni-Morocco, Jijini Dar es Salaam. 

Ndg. Emmanuel amesema ni dhahiri kwamba mradi wa Guardians of the Peak unajikita katika kuutunza Mlima Kilimanjaro, ambao si tu ni urithi wa Taifa bali pia ni alama ya Tanzania katika uwanda wa kimataifa na kupitia Makala ya Guardians of the Peak–Msimu wa Pili, dunia itaweza kuona changamoto za kimazingira na mabadiliko ya tabianchi, umuhimu wa uhifadhi wa maliasili, na jitihada za Tanzania katika kulinda urithi wake wa asili na fursa mbali mbali za utalii endelevu zilizopo Tanzania. 

Aidha, amewahakikishia waandaji wa mradi huu, Guardian of The Peak kwamba serikali kupitia Bodi ya Filamu Tanzania itaendelea kuunga mkono jitihada zao katika mradi huu na miradi mingine inayotumia filamu kama chombo cha mabadiliko chanya, kutoa elimu kwa jamii, na kuitangaza Tanzania kimataifa. 


umetambulishwa rasmi leo Januari 14, 2026, ukiingia katika msimu wake wa pili kwa lengo la kuendeleza juhudi za uhifadhi wa mazingira na kukuza utalii endelevu, hususan katika Mlima Kilimanjaro. Uzinduzi huo unaonesha dhamira ya wadau wa filamu na utalii kutumia sanaa kama nyenzo ya kuhamasisha ulinzi wa mazingira na kuitangaza Tanzania kimataifa.

Kwa upande wake  Mkurugenzi Mtendaji wa Ram Films na mwanzilishi wa mradi huo alisema Guardians of the Peak umeendelea kuwa jukwaa muhimu linalounganisha masuala ya mazingira, ubunifu wa filamu na diplomasia ya watu kwa watu. Alibainisha kuwa mradi huo pia unadumisha na kuimarisha ushirikiano wa kirafiki kati ya Tanzania na China, hususan katika sekta za filamu, utalii na uhifadhi.

Hata hivi  Mkurugenzi huyo ametoa wito kwa wadau wa Filamu na michezo ya kuigiza, taasisi za serikali na sekta binafsi, pamoja na vyombo vya habari kuendelea kuunga mkono mradi huu Guardians of the Peak –Msimu wa Pili na miradi mingine kama hii kwa maslahi mapana ya taifa letu.

Utayarishaji wa Makala ya Guardians of the Peak utaanza rasmi tarehe 20 Januari, 2026.

Comments