BROTHERS ACADEMY 'KUMFUNDISHA' BABA LEVO MASOMO YA SEKONDARI,AJIUNGA NAO

 BROTHERS ACADEMY 'KUMFUNDISHA' BABA LEVO MASOMO YA SEKONDARI,AJIUNGA NAO




Mbunge wa Jimbo la Kigoma mjini Revocatus Chipando maarufu kama Baba Levo ameanza rasmi masomo yake ya sekondari katika taasisi ya Brothers Academy ambapo atasoma elimu hiyo kwa kipindi cha miaka miwili.


Akizungumza na waandishi wa Habari Jijini Dar es salaam mbunge huyo amesema kuwa ameamua kujiunga na Brothers Academy iliyopo Banana,Ukonga Jijini humo ili afikie ndoto zake za kupata elimu mpaka ngazi ya chuo kikuu.

Nimejiunga na Brothers Academy kutokana na kwamba wana programu ya VIP ambayo unaweza kuhudumiwa mahali popote,mimi ni Mbunge,nina kazi nyingi za kuwahudumia Wananchi wa Kigoma Mjini,lakini pia natakiwa kusoma, hivyo hii shule(Brothers Academy)ina programu za kufundisha watu wa VIP kama mimi" amesema Baba Levo.

Aidha ameongeza kuwa Shule ya Brother's Academy inatoa Elimu kuanzia darasa la saba,kidato cha kwanza hadi kidato cha sita kwa muda wa miaka 3,hivyo amewaomba,watu maarufu na Wananchi wote wanaotamani kujiendeleza kimasomo wajiunge na Brothers Academy ili kutimiza ndoto zao.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Brothers Academy Bw.Robert Rwezaula amemshukuru baba levo kwa kijiunga na shule hiyo huku akisisitiza kuwa atapata Elimu iliyo bora kutokana na shule hiyo kuwa na walimu wabobevu.

"Mh.hujakosea kijiunga nasi,na tumekua na bahati kubwa yakua na mtu wa kwanza mashuhuri kwenye shule yetu,ukifanikiwa utakua ni balozi wetu na tunaamini tutapata watu wengi watakaojiunga na shule yetu" amesema Mwalimu Rwezaula.

Aidha amesema kuwa Shule ya Brother's Academy inatoa Elimu kwa gharama nafuu ya kiasi cha shilingi 2500,000 kwa mwaka na hulipwa kwa awamu nne yaani Januari,Aprili,Julai na Septemba.

Comments