CUF YAPINGA MAAMUZI YA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA,POLISI YAWAFUATA NA KUHIMIZA UTULIVU
CUF YAPINGA MAAMUZI YA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA,POLISI YAWAFUATA NA KUHIMIZA UTULIVU

Naibu Katibu Mkuu(CUF) Taifa,Magdalena Sakaya
Na Mwandishi Wetu
Askari Polisi wameingia Ofisi za Makao Makuu ya Chama Cha Wananchi (CUF) Buguruni na kuweka ulinzi mkali baada ya baadhi ya wanaodaiwa kuwa wanachama wao kuingia wakiwa na mabango na matarumbeta
Wanachama hao kwa hali isiyotarajiwa waliingia katika Ofisi za chama hicho wakiwa na mabango ya kumpongeza Msajili wa Vyama Vya Siasa nchini kwa kutengeua uongozi uliopo madarakani chini ya Prof. Ibrahimu Lipumba unaodaiwa kukiuka kanuni za uchaguzi.
Baada ya askari kushuka kwenye gari hilo wakatanda eneo la ndani ya ofisi hizo na askari kiongozi akaenda kuzungumza na wanachama hao na baadaye akaingia ukumbini ambako Sakaya alikuwa akizungumza na waandishi.
Moja kwa moja askari huyo akafika meza kuu na akasema kwa sauti na ninamnukuu....., Sakaya nataka utulivu hapa, nimekuwa na wewe kwenye kampeni bila kuona vurugu,nitashangaa hapa nikiona vurugu,nimepigiwa simu kwamba hapa kuna moto unawaka ndio maana tuko hapa tunataka utulivu, alisikia afande huyo mwenye cheo.
Awali kundi hilo la wanachana wakati linaingia katika ofisi hizo, ikiingia,. Kaimu Katibu Mkuu wa CUF, Magdalena Sakaya alikuwa akizungumza na waandishi wa Habari akipinga uamuzi wa Msajili wa Vyama Vya Siasa kuungeua uongozi uliopo madarakani unaoongozwa na Prof. Lipumba.
Katika Mkutano huo na waandishi wa Habari, Sakaya ameweka wazi uamuzi wa chama hicho kwamba wanakusudia kwenda mahakamani kutafuta haki ya kikatiba uliofanikisha kupitisha viongozi hao.
"Hiki si chama cha kwenye majani, ni chama cha ukombozi na kina katiba, hivyo Msajili hawezi kutuingilia, tunakwenda mahakamani kutafuta haki.
Wanachama wa CUF, hawawezi kuchaguliwa viongozi na Msajili wa Vyama Vya Siasa kwa kufanya hivyo watakuwa wanaleta vurugu na sasa tunaamini wanataka kukiua kama walivyokiua NCCR Mageuzi na vingine vikubwa hapa nchini," amesema.
Msuguano kati ya Msajili wa Vyama Vya Siasa unakuja baada ya CUF, Feb13 mwaka huu kupokea barua inayoyoka Kwa Msajili inayowataka kurejea uchaguzi Mkuu iliyofanyika Desemba mwaka 2024 uliomrejesha kwenye uongozi Prof Lipumba ukiamimika ulikiuka kanuni kutokana kutotimia asilimia 50 za wapiga kura wote.
Aidha Sakaya alihoji kuwa ofisi ya Msajili ilikuwa wapi katika kipindi chote cha miaka miwili iliyopita hadi ije n hoja hizo baada ya kupokea malalamiko Kwa wananchamaa.waliofukuzwa.
Alidai kuwa katika uchaguzi huo, Msajili alikuwepo na alibariki uchaguzi huo hivyo wanashangaa kuona jambo hilo likiibuka sasa.



Comments