RAIS DKT SAMIA KUZINDUA SOKO LA KARIAKOO JUMAPILI HII

 

RAIS DKT SAMIA KUZINDUA SOKO LA KARIAKOO JUMAPILI HII





Na Mwandishi wetu

RAIS  wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan anatarajia kuzindua soko kuu la Kariakoo  Februari 8, 2026 baada ya kukam

Hayo yamebainishwa Jijini Dar es salaam mapema leo Februari 6,2026 na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Albert Chalamila wakati akizugumza na waandishi wa habari.

Amesema  soko hilo kwa sasa limekamilika kwa asilimia 100 ambapo zaidi ya shilingi bilioni 28 zimetumika kukarabati na kujenga soko jipya likiwa na takribani vizimba zaidi ya 1500 kwa ajili ya wafanyabiashara

"Nawaomba  wananchi wakazi wa Mkoa Dar es salaam na wafanyabiashara wadogo wa kati na wakubwa kujitokeza kwenye uzinduzi huo wa Soko la kariakoo ili kumuunga mkono Rais Dokta Samia lakini pia kuweka historia ya tukio hilo kubwa linalotarajiwa kuwa ni kiungo muhimu katika kujenga uchumi wa Mkoa huu na Taifa kwa ujumla"amesema 


Aidha  Chalamila amewataka wafanyabiashara wadogo ambao wamefunga barabara za kuingia soko la kariakoo waondoke na waache barabara hizo wazi kabla ya februari 8 ili kuruhusu wafanyabiashara  kuingia kwenye Soko hilo.

Comments