SBL YAJA NA VIN NKOLOMBOKA,SULUHISHO LA WANAUME
Kinywaji kipya cha Vin Nkolamboka kimezinduliwa rasmi jijini Dar es Salaam katika hafla iliyohusisha wadau mbalimbali wa biashara, sekta ya vinywaji pamoja na wageni waalikwa. Uzinduzi huo umefanyika kwa lengo la kukitambulisha kinywaji hicho katika soko la Tanzania na kutoa chaguo jipya kwa watumiaji wa vinywaji vyenye kilevi.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Meneja Mkuu wa kinywaji hicho, Domivic Salamba, amesema kuwa Vin Nkolamboka ni bidhaa mpya iliyobuniwa kwa kuzingatia mahitaji ya soko la ndani na ladha ya Watanzania. Amesema kampuni yao imewekeza katika ubora wa bidhaa hiyo ili kuhakikisha inakidhi viwango vya kitaifa na kimataifa.
Salamba ameeleza kuwa kinywaji hicho kina kiwango cha kilevi cha asilimia 16, hivyo kimeidhinishwa kutumiwa na watu wenye umri wa kuanzia miaka 18 na kuendelea, kwa mujibu wa sheria na kanuni za nchi. Amesisitiza umuhimu wa matumizi ya kinywaji hicho kwa uwajibikaji ili kuepuka madhara yanayoweza kusababishwa na matumizi kupita kiasi.
Ameongeza kuwa Vin Nkolamboka kimechanganywa na viambato maalum vinavyoongeza nguvu (energy) pamoja na kilevi (alcohol), hatua inayolenga kutoa uzoefu tofauti wa ladha na hisia kwa watumiaji. Kwa mujibu wa meneja huyo, mchanganyiko huo umebuniwa baada ya tafiti za soko zilizobaini kuwa kuna mahitaji ya vinywaji vyenye ladha ya kipekee na athari ya kuongeza nguvu.
Kwa upande wake, baadhi ya wadau wa biashara waliohudhuria uzinduzi huo wamesema kuwa ujio wa Vin Nkolamboka unaongeza ushindani katika soko la vinywaji nchini, jambo ambalo linaweza kusaidia kupanua fursa za biashara na ajira. Wameeleza kuwa bidhaa mpya kama hii zinaweza kuchochea ukuaji wa sekta ya uzalishaji wa vinywaji na kuongeza mapato ya serikali kupitia kodi.
Kampuni inayozalisha Vin Nkolamboka imeahidi kuendelea kufanya kampeni za elimu kwa umma kuhusu matumizi sahihi ya kinywaji hicho pamoja na kuzingatia maadili ya biashara na sheria za nchi. Pia imesema ina mpango wa kusambaza bidhaa hiyo katika mikoa mbalimbali nchini ili kuwafikia wateja wengi zaidi.



Comments