JAFO AWATAKA WAISLAMU KUWATHAMINI WALIMU WA MADRASA,AWAPA MOTISHA
Na Mwandishi wetu, Dar es salaam
Mbunge wa Jimbo la Kisarawe ambaye pia ni mlezi wa taasisi ya Asw-Haabul Kahfi Islamic Center Dkt Seleman Jafo amewataka waumini wa dini ya kiislamu kuwajali walimu wa madrasa kwani wanajitolea kuwajengea misingi Bora watoto wao.
Jafo ameyasema hayo katika mashindano ya 11 ya kuhifadhi Quran tukufu yaliyoandaliwa na Kituo hicho na kufanyika March 7,2026 katika ukumbi wa Paradise Yombo dovya Wilayani Temeke jijini Dar es salaam huku mamia ya waumini wa dini ya kiislamu wakihudhuria.
Amesema walimu wa madrasa wanafanyia Kazi kubwa katika mafundisho hasa ya kitabu kitakatifu Cha Quran hivyo wazazi wanatakiwa kuwakumbuka walimu hao kwani wengi wao wamekuwa wakiishi mazingira magumu.
"hakuna malipo yanayofanana kwa Ile Kazi mnayoifanya walimu wa madrasa kwa Ile Kazi ya mwenyezi Mungu na Allah awalipe kwa wingi wa wema kwa jambo hili mnalolifanya kwa vijana wetu Mungu atuingize katika pepo yake Walimu wa madrasa hawana maisha mazuri hivyo wanatakiwa kujaliwa "alisema.
Hata hivyo katika hatua nyingine Jafo alitoa Shilingi Milioni 5 kwa ajili ya kutoa motisha kwa walimu wa madrasa ambao wanafunzi wao walioshiriki katika mashindano hayo na kufika ngazi ya nusu fainali kwa kutoa laki moja kwa Kila mmoja na laki tatu kwa mwalimu ambaye mwanafunzi wake ameshika nafasi ya kwanza kwenye Kila ngazi za mashindano hayo ya kuhifadhi Quran.
Mmshindi wa kwanza wa juzuu 30 katika mashindano hayo akitangazwa kuwa ni Abdulwahab Daudi aliyepata alama 98.75 aliyeshinda kitita Cha Shilingi Milioni 3 ambapo mashindano hayo yalianzia juzuu moja mpaka 30.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa taaisi hiyo Ustadh Haruna Mbese amesema mashindano hayo yamezidi kukua mwaka Hadi mwaka ambapo kwa mwaka huu wanayafanya kwa msimu wake wa 11 huku akiahidi kuendelea kuboresha zawadi kwa washiriki wa mashindano hayo.



Comments